Kushoto ni Askofu wa Dayosisi ya Rift Valley Mkoani Singida Mchungaji John Daud Lupaana kulia kwake ni Askofu Msaidizi Mchungaji Philemoni Mpilim wakati wa Misa
Afisa Tawala Wilaya ya Ikungi Josephine Gabriel Kadaso akimkaribisha Mkuu wa Wilaya kuzungumza na waumini wa kanisa la Anglikana la Mtakatifu Mathayo-Ikungi, Dayosisi ya Rift Valley, Parish ya Singida
Waumini wakisikiliza kwa makini mahubiri wakati wa uzinduzi wa kanisa la mtakatifu Mathayo
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisalimia na Viongozi mbalimbali wa makanisa ya kikristo muda mchache mara baada ya kuwasili kanisani hapo
Askofu wa Dayosisi ya Rift Valley Mkoani Singida Mchungaji John Daud Lupaa akiwabatiza watoto walioandikishwa kwa ajili ya ubatizo
Katibu wa Dayosisi ya Rift Valley Daud Manase akisoma neno la kwa kutoka Warumi 12:4 wakati wa Misa ya ufunguzi wa kanisa hilo
Waumini wakisikiliza kwa makini mahubiri wakati wa Misa
Jeddy Mzungu akisoma Risala iliyoandaliwa na uongozi wa kanisa mbele ya Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya ikungi Mhe Miraji jumanne MtaturuMkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (kulia), Afisa Tawala Wilaya ya Ikungi Josephine G Kadaso (Katikati) na Kushoto ni Mathias Canal Mwenyekiti wa Taasisi ya Wazo Huru na Mhariri wa Blog ya www.wazo-Huru.blogspot.com wakisikiliza kwa makini mahubiri wakati wa Misa ya ufunguzi wa kanisa la Anglikani Mtakatifu Mathayo-Ikungi, Dayosisi ya Rift Valley, Parish ya Singida
Jamii imeaswa kutofanya ubaguzi wa dini, itikadi,
ama ukabila ili kudumisha msingi imara na ushirikiano madhubuti katika kuimarisha
Amani na Utulivu nchini na kurahisisha shughuli za maendeleo ya kuwahudumia
wananchi kiroho na kidini.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Mhe Miraji Jumanne Mtaturu Amebainisha
hayo wakati wa ufunguzi wa kanisa la Anglikana la Mtakatifu Mathayo-Ikungi, Dayosisi
ya Rift Valley, Parish ya Singida ambapo pamoja na shughuli za kiroho pia
inatoa huduma za kijamii kwa wakazi waMkoa wa Singida ikiwemo huduma za mafunzo
na afya, elimu ya sekondari, Mafunzo ya dini ya kikristo, Hudumaya duka la dawa
pamoja na vituo vya mafunzo kwa watoto walio katika mazingira magumu chini ya
shirika la Compassion.
Dc
Mtaturu amesema kuwa serikali inatambua na kuthamini
mchango wa Taasisi za dini katika kufikia maendeleo ya jamii hivyo wananchi kwa
umoja wao hawapaswi kuwa na sintofahamu kwa sababu ya utofauti wa dini kwani
kufanya hivyo ni kujiweka katika uelekeo wa maendeleo duni kwa Wilaya ya Ikungi
Taifa kwa ujumla.
Aliziomba taasisi za dini kuendelea kushirikiana na
serikali katika ngazi zote kuendelea kudumisha amani na utulivu ili kuendelea
kujenga mazingira mazuri ya jamii kufanya shughuli za kiroho na maendeleo ya kiuchumi
na manufaa ya watanzania wote.
Mtaturu amechangia shilingi milioni mbili kwa kwaya
za Kanisa hilo ili kuimarisha na kutangaza zaidi injili kwa njia ya nyimbo za
kumsifu Mungu wa kweli kwani kupitia uimbaji wananchi wanahamasika na kuachana
na matendo ovu yasiyofaa.
Ametumia nafasi hiyo pia kuwaalika wananchi wote
kuupokea Mwenge wa Uhuru unaotarajia kuwasili wilayani ikungi hapo kesho
ukitokea Wilaya ya Manyoni.
Awali Askofu wa Dayosisi ya Rift Valley Mchungaji
John Daud Lupaa wakati wa mahubiri alisema kuwa viungo vya mwili wa binadamu
vinaushirikiano kuliko hata Viongozi wa Umoja wa mataifa hivyo kupitia mfano
huo amewasihi viongozi wa dini, waumini na watumishi wa serikali kushirikiana
kwa pamoja katika kuimarisha na kuitangaza dini kwani ndio njia pekee ya
kuwafanya watanzania kusonga mbele katika shughuli za maendeleo.
Sambamba na hayo pia amempongeza Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kwa juhudi na utendaji uliotukuka kwa
kuimarisha amani na uwajibikaji kwa kuwaagiza watumishi wote wa Umma kuhamia
Wilayani hapo ili kuwa karibu na maeneo yao ya kazi na kuimarisha uchumi wa
Wilaya.
Akisoma risala ya ufunguzi wa kanisa hilo Jeddy Mzungu
alisema kuwa Malengo ya Dayosisi hiyo ni kuhakikisha inafanya kazi za jamii ili
kuwafikia wakazi wote wa Mkoa wa Singida na kuwasaidia wananchi kuzitambua
rasilimali walizonazo na kuwajengea uwezo ili waweze kuzitumia ipasavyo katika
kujikwamua kiuchumi.
Kanisa la Anglikana na Mtakatifu Mathayo Ikungi
lilianza mwezi disemba mwaka 1989 chini ya mwasisi Mchungaji Stear Mapunda
kufuatia shinikizo la watumishi wanane wa serikali ambao walikuwa ni
waanglikana.
Pamoja na Mtazamo huo pia wameiomba serikali
kulisaidia kanisa hilo katika ujenzi wa jingo la shule ya Msingi Mbwanjiki
ambapo pia mkuu wa wilaya hiyo amewasihi kufanya tathmini ya gharama
inayohitajika na hatimaye kuiwasilisha Ofisini kwake kwa ajili ya ushirikiano
wa kukamilisha ujenzi wa shule hiyo.
0 comments:
Post a Comment