METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, June 23, 2023

VIJIJI VYOTE AMBAVYO VIPO KWENYE MRADI WA REA AWAMU YA 3 MZUNGUKO WA 2 KUKAMILIKA DISEMBA 2023



Na Saida Issa, Dodoma 

SERIKALI imesema kuwa Vijiji vyote ambavyo vipo kwenye Mradi wa REA awamu ya 3 mzunguko wa pili vitakamiloka ifikapo disemba mwaka huu 2023. 

Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati Steven Byabato alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbeya Vijijini Oran Njeza alipouliza Je, ni lini Serikali itapelekea umeme kwenye vijiji vya kata ya shizuvi ambavyo ni sehemu ya Rea awamu ya 3 mzunguko wa pili? 

"Vijiji vyote ambavyo vipo kwenye mradi wa   REA awamu ya tatu mzunguko wa pili vitakamilika ifikapo disemba mwaka huu 2023, 

Nimuhakikishie Mheshimiwa Orani Njeza kwamba vijiji hivyo pia katika kata hizo vitakuwa vimefikiwa umeme kabla ya disemba mwaka huu,"amesema Naibu Byabato. 

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com