METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, March 8, 2023

WANAWAKE TANESCO KAGERA WAONYESHA UMAHILI WAO KWA KUFANYA KAZI ZA WANAUME


Watumishi wa shirika la umeme Tanzania TANESCO mkoa wa Kagera wameadhimisha siku ya wanawake Duniani kwa kusimika nguzo za umeme katika maeneo mbalimbali Kazi iliyozoeleka kufanywa na wanaume.

Wakiongea na  kwa nyakati tofauti watumishi hao wamesema kuwa wameamua kufanya hivyo ILI kunonyesha jamii kuwa Kazi zinazofanywa na wanaume hata wanawake wanaweza kuzifanya pia.

Wamesema kuwa wanamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwapa nafasi wanawake katika serikali yake hivyo nawao wameahidi hawatamuangusha katika kuhakikisha dhamila yake na imaani yake kwa wanawake inatimia.

Aidha sambamba na kusimika nguzo za umeme watumishi hao pia wameshiriki zoezi la kupanda miti katika shule ya sekondari Rugambwa ambayo ni shule ya wasichana kwa lengo na kuwapa moyo watoto wakike wanaosoma shule hiyo kuwa wakiamua wanaweza kutimiza ndiyo zao.

Sehemu nyingine iliyopandwa miti ni shule yaa sekondari Kagemu iliyopo Manispaa ya Bukoba ikiwa pia ni ishara ya kusisitiza utunzaji wa mazingira.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com