METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, October 7, 2022

WATUMISHI WA TANESCO WATAKIWA KUFANYA KWA ARI NA KUJITUMA

Mwakilishi wa mkurungezi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira TUWASA Namyaki Molel akikata keki ambapo kushoto kwake ni meneja wa shirika hilo mkoa wa Tabora mhandisi Khadija Mbarouk ,kulia ni afisa uhusiano mkoani Tabora Witness Msumba na huyo mwanaume ni  mkurungezi wa Tanesco kanda ya magharibi Mhandisi Richard Swai. Meneja wa shirika hilo mkoa wa Tabora mhandisi Khadija Mbarouk alipokuwa akitoa huduma kwa wateja wa nje leo mjini hapa

Na Lucas Raphael,Tabora

Watumishi wa shirika la la umeme  ( Tanesco) Mkoani Tabora wametakiwa kufanya kazi kwa ari, ushirikiano ,ubunifu na kujituma kwa hali ya juu ili kuweza kutimiza malengo ya Serikali  kwa wateja yanafikiwa.

Kauli hiyo imetolewa na meneja wa shirika hilo mkoa wa Tabora mhandisi Khadija Mbarouk wakati  hafla fupi ya kuwapongeza wateja waliofanya vizuri kwa ulipa wa bili za umeme iliyofanyika  octoba 7 katika ofisi za shirika hilo mjini hapa.

Alisema kwamba kutokana na shirika kupitia katika mifumo  mipya ya kidigtali wanapaswa kwenda na kasi na viwango katika kutoa huduma iliyobora kwa wateja wao.

Mhandisi huyo alisema wanatakiwa kwenda sambamba na kasi ya ubunifu  ili kuweza kutimiza malengo ya Serikali kwa wananchi na wadau wengine ambao ndio wateja wao yanafikiwa.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurungezi wa Tanesco kanda ya Mahgaribi Mhandisi Richard Swai aliwataka watumishi wa shirika hilo kuahikisha wanatoa huduma kwa wakati mfupi ili kutomchosha mteja.

Mhandisi Swai alisema kwamba Tanesco wamejiweka malengo ya kuwafikia wateja walioomba huduma hiyo na kuwaunganishia umeme kutoka siku 15 hadi siku saba baada ya kulipia.kwani hivi sasa mifumo imebadilika na kuingia kidigtali.

Naye mwakilishi wa mkurungezi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira TUWASA Namyaki Molel alilishukuru shirika la umeme mkoani Tabora kwa kutambua mchango wao kwa kulipia bila zao kwa wakati.

Alisema kwamba licha ya kulipia bili zao kwa wakati lakini wanaitaji watu wengi kuwekeza mkoani Tabora kutokana na kuwa na maji ya uhakika kwa asilimia 100.

Wiki  ya huduma kwa mteja inaadhimishwa kila mwaka kuanzia wiki ya kwanza ya mwezi octoba.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com