Na Mathias Canal, WEST-Mwanza
Serikali
imetumia Shilingi Bilioni 1 kwa ajili ya kukarabati na kuongeza miundombinu ya
elimu ya Chuo cha Ualimu Butimba kilichopo katika Wilaya ya Nyamagana Mkoani
Mwanza.
Butimba
ni kati ya Vyuo vilivyonufaika na jitihada za serikali katika kuimarisha sekta
ya elimu huku uongozi wa chuo hicho ukipongezwa kwa usimamizi madhubuti wa
rasilimali fedha.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda ameyasema hayo tarehe 7
Octoba 2022 wakati akizungumza na Menejimenti na watumishi wa Chuo cha Ualimu
Butimba wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza.
Waziri
Mkenda amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu
Hassan kwa kuimarisha sekta ya elimu kwani muelekeo wa serikali katika kuwekeza
kwenye sekta ya elimu umezidi kuimarika maradufu.
“Tusiposema
watu wanasahau, Mazuri yanafanyika halafu tunasahau na muelekea wa serikali ya
awamu ya sita ni kupeleka fedha nyingi zaidi kwenye miradi ya maendeleo katika
Halmashauri” Amekaririwa Waziri Mkenda
Amewataka
walimu na watumishi wote wa Chuo hicho kuhakikisha kuwa wanaunga mkono juhudi
za serikali kwenye sekta ya elimu na shughuli zote za maendeleo huku
akisisitiza kuwa changamoto katika sekta ya elimu haziwezi kukosekana lakini
serikali inaendelea kuzitafutia ufumbuzi.
Waziri
Mkenda ameutaka uongozi wa Chuo cha Ualimu Butimba kuhakikisha kuwa unaendelea
kusimamia miradi kwa uaminifu mkubwa huku akiupongeza kwa matumizi mazuri ya
fedha zote za miradi.
Kadhalika Waziri Mkenda amempongeza Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza Mhe Stanslaus Mabula kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya ya kuhamasisha shughuli za maendeleo katika jimbo lake hususani miradi ya elimu.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment