METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, October 11, 2022

RAIS SAMIA ANAWEPENDA, MSIOGOPE


 





NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi amewataka watumishi wa umma nchini kutoogopa kutoa malalamiko yao na kueleza changamoto zao kwa viongozi wao ili kuweza kutatuliwa na kuacha kuwa waoga kwani Rais Samia Suluhu Hassan ni Kiongozi mpenda haki.

Ndejembi ametoa kauli hiyo wakati akiwa kwenye ziara yake ya kuzungumza na watumishi wa umma katika Manispaa ya Wilaya ya Lindi na Halmashauri ya Wilaya ya Mtama.

Akizungumza na watumishi hao, Naibu Waziri Ndejembi amewataka kuacha kuwa na uwoga wanapoona viongozi wa kitaifa wamewatembelea na badala yake waeleze changamoto zinazowakabili ili ziweze kutatuliwa.

" Ofisi ya Rais Utumishi kwa kutambua thamani ya watumishi wa umma ndio maana tunafanya ziara za kuja huku chini kuwasikiliza nyinyi ambao ndio watoa huduma na watendaji wa serikali kwa wananchi huku chini, niwaombe msiogope elezeni changamoto zenu na Serikali ya awamu ya Sita ya Rais Samia ipo tayari kuzitatua zote lengo ni kuhakikisha watumishi wa umma wanafanya kazi kwenye mazingira bora.

Niwaase pia kuheshimiana kwenye maeneo yenu ya kazi, Mkubwa amheshimu mdogo na mdogo amheshimu mkubwa, wote hapa mmekutanishwa na kazi, kazi ya kuwatumikia watanzania, Serikali haitotaka kuona kuna makundi kwenye maeneo ya kazi, Wote mna jukumu la kumsaidia kazi Rais Samia katika kuwatumikia watanzania.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com