METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, July 31, 2022

WAZIRI AWESO ATAKA VIONGOZI WA MABONDE YA MAJI KUSHIRIKISHA WANANCHI ILI KUTUNZA VYANZO VYA MAJI ALIPONGEZA BONDE LA KATI






Waziri wa Maji Jumaa Aweso (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa wa ujenzi wa ofisi ya maabara ya bodi ya maji Bonde la Kati, mjini Singida leo Julai, 30, 2022. Kutoka kulia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu, Afisa wa Bodi ya Maji Bonde la Kati, Mhandisi Danford Samson, Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Mulagiri, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Singida, Lusia Mwiru na Mjumbe wa Siasa Mkoa wa Singida, Diana Chilolo.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizindua jengohilo lililopo Kata ya Utemini mjini Singida.

Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji Nchini Dk. George Lugomela akitoa taarifa ya mradi huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Taifa, Mhandisi Mbogo Futakamba akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Bonde la Kati, William Mabula akizungumza kwenye hafla hiyo.
Waziri wa Maji Juma Aweso (katikati) akitoka kukagua maabara ya maji. 
 Afisa wa Bodi ya Maji Bonde la Kati, Mhandisi Danford Samson akiwatambulisha viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo.

Hafla hiyo ikiendelea.

Kwaya ya Chuo cha Utumishi wa Umma Mkoa wa Singida ikitoa burudani.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu, akizungumza kwenye uzinduzi huo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Bonde la Kati aliyemaliza muda wake. Mhandisi Samson Mabala akizungumza kwenye hafla.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhandisi Paskas Mulagiri akizungumza kwenye hafla hiyo.
Wajumbe wa Bodi ya Maji Bonde la Kati waliomaliza muda wao wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Bonde la Kati, William Mabula akionesha zana za kazi baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Maji Jumaa Aweso.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso (kushoto) akikagua ujenzi wa mradi wa maji, Dareda, Singu, Sigino na Bagara unaotekelezwa Mkoa wa Manyara ambao utagharimu Sh.12 Bilioni.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Manyara (BAWASA) Idd Msuya (katikati) akimuelezea Waziri wa Maji Jumaa Aweso kuhusu mradi huo.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso (kushoto) akipata maelezo ya ujenzi wa mradi ya ofisi ndogo ya Bodi ya Maji Bonde la Kati inayojengwa Babati mkoani Manyara ambao ujenzi wake utagharimu zaidi ya Sh.700 Milioni. Katikati ni Afisa Maji Bodi ya Maji Bonde la Kati, Mhandisi Danford Samson.

 

Na Hamis Hussein ,Singida

 
WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewataka viongozi wote wa mabonde yote tisa ya maji  nchini  kushirikisha wananchi katika utunzaji, uanzishaji, na uendelezaji wa rasilimali za maji ili kuondoa changamoto zinazoathiri Rasilimali hiyo na vyanzo vyake. 

Mhe. Aweso amesema hayo Julai 30, 2022 mjini Singida baada ya kufungua jengo la ofisi ya bodi ya maji bonde la kati ambalo ujenzi wake umegharimu zaidi ya Sh.bilioni 2.9 hadi kukamilika kwake, alisema ushirikishaji  wa utunzaji wa vyanzo vya maji ni jambo shirikishi.
" Suala la utunzaji na ulindaji wa vyanzo vya maji ni shirikishi, tumeona baadhi ya lazima tusaidiane kwa pamoja tumeona baadhi ya watu wa bonde mara nyingi wanachukua hatua  baada ya jambo kuwa limetokea , umesikia tuu kwenye vyombo vya habari kuwa waziri amesema hivi unachukua  panga unakata mahidi ya watu hilo haliwezekani" .alisema Mhe. Aweso.

Aliongeza kuwa Bonde la kati limekuwa likishirikisha jamii katika utunzaji wa vyanzo vya maji akitolea mfano namna bonde hilo lilivyoweza kushirikiana na wananchi wa Karatu mkoani Arusha ambapo limejenga Mabirika ya kunyweshea Mifungo kutunza vyanzo vya maji.

"Bonde la kati mmetupa somo kuwa jamii ipo tuu ukiishirikia utafanikiwa na usipoishirikisha utakwama, sasa hivi mmejenga mabirika huko karatu sasa wafugaji wanatumia kunyweshea mifugo yao piga makofi kwa bonde la kati na wengine waige waje wajifunze bonde la kati" alisema Mhe. Aweso.

Aweso alisema Bodi za Maji zihakikishe zinawatambua na kuwashirikisha watumiaji wa maji kwani wapo baadhi wanatumia maji bila kuwa na vibari lakini hawatambuliwi.

"Moja ya changamoto ya mabonde yetu yanatumika tu kwa ajili ya 'ambush' tu, washirikisheni, watambuweni wadau wenu wa maji na msiweke bei za kuwakandamiza, wekeni bei rafiki," alisema.

Aidha Mhe. Aweso alifika hadi unapojengwa mradi wa maji wa Dareda Singu Sigino Baraga mkoani Manyara ambapo alimwagiza katibu mkuu wa zwizara ya maji Mhandisi Antony Sanga kupeleka shilingi Bilioni 2.3 ili kukamilisha ujenzi wa mradi huo ambao unatizamiwa kugharimu sh. bilioni 12

Kuhusu upatikanaji wa maji nchini Mhe. aweso alisema kuwa wizara yake inaendelea kuhakikisha inatekeleza kwa vitendo upatikanaji wa maji yenye kutoshereza na kuwayaaiga mabonde yote ya maji kuzipitia upya takwimu za upatikanaji wa  maji ukilinganishwa na hali halisi ya watu iliyopo hivi sasa.
" Baada ya sensa  takwimu hizi za upatikanaji wa maji zirejewe , tunapozungumza tuna mita za ujazo bilioni  126 sasa tunaongezeko la watu je  rasilimali zetu za maji zipokwa kiwango kile?" Alisema Mhe. Aweso.

Waziri Aweso alisema ni muda mwafaka rasilimali za maji kwa maana ya mvua isiwe kama laana bali iwe baraka na fursa kwa maji ya mvua kuvunwa kwa kujenga mabwawa ya kimkakati ili maji hayo yatumike kwa matumizi ya kunywa.

Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji Dk.George Lugomela alisema Bodi ya Maji Bonde la Kati iliyomaliza muda wake imejitahidi kufanya kazi ambapo imeongeza ukusanyaji wa mapato kutoka Sh.Milioni 300 zilizokiwa zikikusanywa awali na kufikia Sh.mil.800.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhandisi Pakas Muragili, alisema Bonde ndio injini ya maji hivyo serikali kupitia wizara ya maji iyawezeshe mabonde ya maji nchini ili yafanye utafiti wa juu ya upatikanaji wa rasilimali za maji katika kila kijiji au mtaa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Bonde la Kati, William Mabula alisema  katika kipindi cha uongozi wake watahakikisha wanakuwa karibu na jamii ya watumia maji ikiwa ni pamoja na kuwapatia vibari kwa njia rafiki, kusimamia rasilimali za maji na kuongeza mapato kutoka Sh.milioni 800 hadi kufikia Sh. Bilioni 1.

 

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com