Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kibakwe katika mkutano wa Hadhara uliofanyika katika tarafa ya Kibakwe Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Josephat Maganga mapema leo alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene (kulia) akizungumza na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mpwapwa Bi, Mwanahamisi Ally katika mkutano wa Hadhara ulioufanyika Tarafa ya Kibakwe katika Halmashauri ya Mpwapwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene akizungumza na halaiki ya wananchi walijitokeza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Jimbo la Kibakwe Wilaya ya Mpwapwa Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amesema katika kipindi cha Mwaka Mmoja wa Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi Billion kumi kwa Halmashauri ya Mpwapwa kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo
“Unapopeleka fedha kwa wanachi kule chini, kule chini ndio kuna chanagamoto na wananchi wetu ndio wanapata maendeleo, miradi ili tuliyopewa mwaka jana lazima tuitekeleze kwa kasi kubwa, ili zinapokuja fedha nyingine tuendelee kutekeleza miradi”
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe. George Simbachawene Mbunge wa Kibakwe wakati akihutubia wananchi wa Jimbo la Kibakwe wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.
“Wananchi wa Mpwapwa sasa wanazungumza kuhusu maendeleo nawapongeza kwa kuwa wanaharakati wa maendeleo, alisema Mhe Waziri”
Aidha Mhe. Simbachawene amewahakikisha wananchi wa Kata kibakwe kwamba Jokofu kwa ajili ya Kuhifadhi maiti lipo, katika gharama za ujenzi wa kituo cha Afya kibakwe.
Naye Diwani wa Kata ya Kibakwe Mhe David Atanas amepongeza jitihada zinazofanywa na Mbunge wa jimbo la kibakwe katika kuletea wananchi maendeleo, amesema kibwakwe imepata million 500 kwa ajili ya ujenzi miundo mbinu ya maji. Katika jimbo la kibakwe ujenzi wa barabara kwa umbali wa km 1.
0 comments:
Post a Comment