Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Innocent Bashungwa katikati akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za ubora wa Taaluma kwa Matokeo ya Mtihani wa kumaliza Elimu Msingi, Kidato cha Nne na Sita iliyofanyika Jijini Dodoma leo February 11 2022.
Wanafunzi na wadau wengine wa Elimu wakiwa katika hafla ya Utoaji tuzo jijini Dodoma.
Waziri wa Tamisemi Mhe . Innocent Bashungwa Akizungumza katika halfa ya utoaji tuzo za Ubora wa Taaluma kwa Elimu Msingi na Sekondari.
Naibu waziri wa Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe.David silinde akizungmza na washirikia katika hafla ya utoaji tuzo za ubora Elimu nchini Jijini Dodoma
Wadau wa Elimu na Viongozi Mbalimbali wakifuatilia Zoezi la utoaji Tuzo za Ubora wa Elimu
Mhe. Waziri Bashungwa Akihutubia umma kwenye utoaji wa tuzo Jijini Dodoma.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Antony Mtaka Akizungumza na Wanafunzi , Viongozi na Wadau wengine wa Elimu Kwenye Hafla ya Utoaji Tuzo za Ubora Elimu .
Hafla ya Utoaji Tuzo ikiendelea.
Na
Mathias Canal - Dodoma
MPANGO
wa Elimu bila Malipo, ambao ulianza kutekelezwa na Serikali kuanzia Desemba,
2015, kwa kuzingatia Sera ya Elimu ya Mwaka 2014, Ibara ya 3.1.5 na Ibara ya
52(a) ya Ilani ya Uchaguzi, ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015. Mpaka sasa,
Serikali imepeleka jumla ya shilingi trilioni 1.43, kwa ajili ya kugharamia
Mpango wa Elimumsingi bila Malipo.
Mpango
wa Elimu msingi bila malipo umeleta fursa ya upatikanaji wa Elimu kwa kuongeza
uandikishaji wa wanafunzi, kutokana na kuondolewa kwa vikwazo. Katika mwaka
2016, jumla ya wanafunzi 2,670,125 waliandikishwa, kati ya hao wanafunzi
917,137 wa elimu ya awali, 1,386,592 wa darasa la kwanza na wanafunzi 366,396
wa kidato cha kwanza.
Kwa
mwaka 2022, jumla ya wanafunzi 3,046,919 wameandikishwa, kati ya hao wanafunzi
1,123,800 ni wa Elimu ya Awali sawa na asilimia 82, wakiwemo wenye mahitaji
maalum 2,352, wanafunzi 1,454,544 ni wa darasa la kwanza sawa asilimia 91, na
wanafunzi 664,698 wakiwemo wenye mahitaji maalum 2,747, wanafunzi 664,698 wa
kidato cha kwanza wameripoti shuleni, sawa na asilimia 73.2 ya wanafunzi
waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza Mwaka 2022, wakiwemo wanafunzi 679
wenye mahitaji maalum.
Serikali
imefanya jitihada kubwa kuongeza miundombinu ya shule kupitia program na miradi
mbalimbali inayotekelezwa nchini. Serikali imekamilisha ujenzi wa vyumba vya
madarasa 3,000 katika Vituo shikizi vya shule za Msingi, madaraza 12,000 katika
shule za sekondari na mabweni 50 kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum
kupitia mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO -
19 (TCRP).
Vilevile
Serikali imekamilisha vyumba vya madarasa 560 kupitia tozo za miamala ya simu.
Aidha, Serikali imepeleka fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa ajili
ya ujenzi wa shule mpya 235 za kata na shule 10 za kitaifa za wasichana za
Mikoa kupitia mradi wa SEQUIP. Serikali imekuwa ikijenga nyumba za walimu
kupitia programu zake mbalimbali kama vile GPE-LANES na EP4R.
Serikali
inatambua mchango mkubwa unaofanywa na walimu nchini katika kuboresha taaluma,
hivyo ni dhamira ya Serikali kuendelea na ujenzi wa nyumba za walimu kulingana
na bajeti.
Serikali
ya Awamu ya Sita imeendelea kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji
katika Shule za Msingi na Sekondari Nchini. Kwa Mwaka 2021 ufaulu katika
mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi umefikia asilimia 81.97, mtihani wa
kumaliza kidato cha nne umefikia asilimia 87.30 na kidato cha sita asilimia
99.62.
“Ninawapongeza kwa kuongeza na
kuimarisha ufaulu. Hata hivyo nina wahimiza kuongeza usimamizi wa shughuli za
Elimu na kuondoa changamoto zinazosababisha baadhi ya shule kutofanya vizuri”
Katika
kuimarisha utendaji kazi, mipango madhubuti imewekwa ili kuhakikisha walimu,
wakuu wa shule, Maafisa Elimu wa Kata, Wilaya na Mikoa wanaendelea kupata mafunzo
mbalimbali ya kuwajengea uwezo katika ufundishaji na usimamizi wa Sekta ya
Elimu.
Katika
mwaka wa fedha 2020/2021 jumla ya walimu 1,817 wanaofundisha wanafunzi wenye
mahitaji maalum ya ujifunzaji, wamejengewa uwezo wa kutumia mbinu za
kufundishia na kujifunzia. Vilevile walimu Wakuu 8,096 walipata mafunzo juu ya
matumizi ya Kiunzi cha Uthibiti Ubora wa Shule ili kuhakikisha Uthibiti wa
Ubora wa Shule unakuwa na matokeo mazuri, kuanzia katika ngazi ya Shule.
Mafunzo yataendelea kutolewa kila mwaka ili kutimiza lengo la kumarisha
utendaji kazi.
Serikali
imeanzisha mifumo ya Kielektroniki ili kuboresha na kurahisisha shughuli za
utendaji kazi. Pamoja na mifumo mingine, Mfumo maalumu wa kielektroniki kwa
ajili ya kukusanya na kuratibu madai/madeni ya walimu (Maden-MIS) umebuniwa na
Ofisi ya Rais – TAMISEMI.
Mfumo
huu unarahisisha ukusanyaji wa madeni ya walimu yasiyo ya mishahara ambapo,
Mwalimu anaingiza madai yake mahali popote alipo na taarifa za madai hayo,
zinafika katika mamlaka kwa muda mfupi na kutoa mrejesho.
Lengo
la kuanzisha mfumo huu ni kurahisisha ulipaji wa madeni ya walimu. Ipo mifumo
mingine katika sekta ya elimu hivyo, nawahimiza kuitumia mifumo hii ipasavyo
kwa manufaa ya sekta ya Elimu.
” Leo hii tunatoa tuzo kwa Mikoa,
Halmashauri, Walimu na wanafunzi waliofanya vizuri zaidi, katika taaluma kwa
mwaka 2021. Kauli mbiu isemayo kuwa ‘Uboreshaji wa Ufundishaji na Ujifunzaji
shuleni ni chachu ya kuongeza kiwango cha ufaulu wa Wanafunzi’, inathibitisha
maelezo ya hali halisi iliyopo sasa, katika Sekta ya Elimu”
Napenda
kuchukua fursa hii sasa kutoa maelekezo na kusisitiza mambo muhimu yafuatayo; -
i.Kuhakikisha
mnafuata sheria, miongozo na taratibu katika usimamizi wa sekta ya Elimu ili
kufikia malengo ya Serikali;
ii.Kuhakikisha
mnasimamia vizuri miradi yote, inayotekelezwa katika maeneo yenu, ili kuwa na
miradi yenye viwango, ukilinganisha na thamani ya fedha;
iii.Kuhakikisha
majengo yote ya Serikali, ikiwemo mali za shule vinatunzwa vizuri, ili kuweza
kudumu kwa miaka mingi na kutumika na vizazi vijavyo;
iv.Kuhakikisha
mnakuwa kiungo kizuri, kati ya viongozi walioko katika maeneo yenu na jamii,
jambo ambalo litawawezesha kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi. Wapo
baadhi yenu hawana mahusiano mazuri na jamii, hivyo kukwamisha utekelezaji wa
baadhi ya shughuli za serikali;
v.Kuhakikisha
mnandaa motisha kwa walimu, na wanafunzi ili kujenga ari ya ushindani, wakati
wote wa kutekeleza sera ya elimu nchini.
vi.Kuhamasisha
jamii iweze kutoa chakula kwa wanafunzi wote.
Serikali
itaendelea kutoa Elimumsingi Bila malipo, kuboresha miundombinu, na kusambaza
vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
Niwasisitize
muendelee kuchapa kazi kwa moyo wa uzalendo, bidii, maarifa na ushirikiano ili
tuweze kufikia malengo katika Kuboresha Elimu Nchini.
Ninahitimisha
hotuba yangu kwa kusema “Uboreshaji wa ufundishaji na ujifunzaji shuleni ni
chachu ya kuongeza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi”
0 comments:
Post a Comment