METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, December 20, 2021

WALIOSHINDWA TUZO ZA FILAMU WASIKATE TAMAA

   

ADELADIUS MAKWEGA–WUSM MBEYA

Rais wa Shirikisho la filamu nchini Elia Mjata amesema kufanyika kwa kilele cha Tuzo za Filamu mkoani Mbeya kumethibitisha kuwa sasa matamasha mengi ya Sanaa na Michezo na hata Utamaduni yanaweza kufanyika maeneo yoyote taifa letu sikama ilivyozoeleka kufanyika Dar es Salaam tu.

Kauli ya Rais huyo wa Shirikisho la Filamu nchini imetolewa usiku wa Disemba 18, 2021 Jijini Mbeya ambapo wasanii zaidi ya 30 na viongozi wa kitaifa wanne wa Tanzania walitukiwa tuzo hizo za filamu nchini.

“Watu wengi mwanzoni waliguna tuzo hizo kufanyika Mbeya lakini sasa imethibitsha kuwa inawezekana na kasumba ya kila jambo Dar es Salaam inatoweka.”

Kiongozi huyo wa filamu nchini aliomba ushirikiano wa mashirikisho mengine ya sanaa na michezo nchini na amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa uteuzi wa vijana katika nafasi mbalimbali kwani wanatoa ushirikiano mzuri kwa wasanii.

“Tuzo hizo za filamu zinatolewa kwa haki na kwa walioshindwa msikate tamaa ninawashauri muendelee kushiriki mwakani ambapo tunatarajia kuyafanya katika mkoa mwingine wa taifa letu.”

Washiriki zaidi ya 660 wa filamu waliwasilisha kazi zao, wakachujwa na kupata kazi 90 katika kazi hizo wakatengwa katika makundi ya watatu watatu na kupatikana washindi 30 huku ikitarajiwa mwakani idadi ya kazi zitakazopokelewa kuongezeka maradufu.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com