METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, August 27, 2021

DC MOYO:WIZI,UDUMAVU,UBADHIRIFU WA MALI ZA UMMA NA UKATILI WA KIJINSIA HAVIKUBARIKI IRINGA

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo  akiwa kwenye mmoja ya mkutano wa hadhara alipokuwa ameanza ziara ya kutembelea vijiji 137 vya wilaya hiyo

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kata ya Itunundu

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo  akiwa kwenye mmoja ya mkutano wa hadhara alipokuwa ameanza ziara ya kutembelea vijiji 137 vya wilaya hiyo.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

WANANCHI wa wilaya ya Iringa wametakiwa kuhakikisha wanashiriki kudhibiti wizi,udumavu,ubadhirifu wa mali za UMMA,kuacha mara moja kufanya ukatili wa kijinsia,kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona,kuacha tabia ya kuharibu miundombinu ya barabara na mtandao wa maji kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo kwa kasi inayotakiwa kutokana na shughuli za kiuchumi wanazozifanya wananchi.

Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea vijiji 37 vya wilaya ya Iringa kwa lengo la kusikiliza na kuzipatia ufumbuzi kero mbalimbali zinazowakabili wananchi,Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa ziara hiyo itakuwa na kauli mbiu inayosema ulipo nipo sema kweli acha majungu ikiwa na lengo la kuwasikiliza na kutatua changamoto za wananchi wa wilaya ya Iringa.

Moyo alisema kuwa ameenza rasmi ziara ya kusikiliza kero za wananchi katika kata ya Itunundu kwa kutembelea vijiji vitatu ambavyo ni Itunundu,kimande na Mbuyuni kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi kero hizo.

Alisema kuwa katika ziara hiyo alibaini kuwa wananchi wa vijiji hivyo wamekuwa wakilalamikia tatizo la ubovu wa miundombinu ya umwagiliaji wa skim za kata hiyo ambazo ndio zimekuwa uti wa mgongo wa uchumi kwa wananchi wa kata hiyo.

Moyo alisema kuwa kunachangamoto ya kuharibika kwa skimu ya mlenge ambayo serikali imeanza kutafutia ufumbuzi kwa kuwaleta wataalam na fedha tayari zipo kwa ajili ya kutatua tatizo la skimu hiyo hivyo aliwatoa hofu wananchi juu ya skimu hiyo.

Alisema kuwa kumeibuka tatizo la viongozi wa vijiji hivyo kuuza nyasi kwa wafugaji za kwenye mabonde bila kuwashirikisha wakulima na wananchi kwa ujumla kwa kuwa wao ndio wenye mali hizo.

Moyo aliwataka viongozi wote wa vijiji hivyo kuhakikisha wanafanya kazi kwa kushirikiana na wananchi ili kuondoa changamoto ambazo zimekuwa zikirudisha nyuma maendeleo ya wananchi bila sababu yeyote ile.

Aidha Moyo alisema kuwa wilaya ya Iringa bila wizi,udumavu,ubadhirifu wa mali za UMMA, ukatili wa kijinsia, tabia ya kuharibu miundombinu ya barabara na mtandao wa maji inawezekana na kuifanya wilaya ya Iringa kuwa wilaya ya kuigwa hapa nchini.

Lakini mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alifanikiwa kutatua changamoto za wananchi ambao walifika kwenye mikutano ya hadhara na kutoa kero zao na mikutano ya vijiji hivyo vitatu vilifanikiwa kuhudhuriwa na wananchi wengi ambao walitoa kero mbalimbali na wakaridhika na namna ambavyo mkuu wa wilaya aliyokuwa anatoa majibu ya maswali yao.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Itunundu Jellah Lukinga alisema kuwa serikali imetenga kiasi cha shilingi milioni mia moja (100) kwa ajili ya kutatua changamoto ya mfereji wa Mlenge na wataalam kutoka katika wizara  ya Kilimo tayari wameshafika  kwa ajili ya kufanya tasmini na kutafuta njia mbadala ya kudumu ya mfereji huo ambao umekuwa uti wa mgongo wa uchumi wa wananchi wa kata hiyo.

Lukinga alisema kuwa kuharibika mara kwa mara kwa mferji huo umekuwa ukirudisha nyuma maendeleo ya wakulima wa kata hiyo hivyo watafiti hao wamefika kwenye eneo la mradi ili kutafuta njia ya kutatua kero hiyo ambayo imekuwa ikisumbua mara kwa mara.

Alisema kuwa iwapo wataalamu kutoka wizara ya kilimo wakifanikiwa kutafuta njia ya kudumu ya tatizo la mfereji wa mlenge basi watakuwa wamesaidia kukuza uchumi wa wananchi wa kati hiyo,tarafa na wilaya na mkoa wa Iringa kwa ujumla.

Nao baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mikutano ya mkuu wa wilaya huyo Mohamed Hassan Moyo walisema kuwa wamefarijika kuona namna ambavyo mkuu wa wilaya ametatua changamoto za wananchi na kuzimaliza kwa hoja zenye mashiko ambazo wao kama wananchi wameridhika nazo kwa kiasi kikubwa. 

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com