METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, February 19, 2021

RUWASA KAGERA KUWAFUNGIA WANANCHI MAJI MAJUMBANI BURE, WENYEVITI WA HALMASHAURI WACHEKELEA

   

Wakala wa Maji Vijijini RUWASA Mkoani Kagera ipanga kuanzisha mpango wa kuwasogezea huduma ya maji wananchi majumbani ili kuweza kuwapunguzia adha kubwa ambayo wamekuwa wakiipata kufata maji kwenye maeneo mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa RUWASA Mkoani humo Mhandisi Warioba Sanya wakati wa kikao Cha menejimenti ya RUWASA na wenyeviti wa halmashauri zote za mkoa wa Kagera pamona na makatibu tawala kilichofanyiwa February 18, mwkaa huu katika ukumbi wa Maanispaa ya Bukoba.

Mhandisi Sanya alitoa kauli hiyo wakati akiwasilisha mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2021/2022 iliyolenga kutoa mwanga wa namna walivyojipanga kuhakikisha miradi mbalimbali ya maji Mkoani humo inakamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Amesema kuwa kwaSasa wameanzisha utaratibu wa kila wanapojenga mradi waneweka sehemu ya kuwaunganishia wananchi maji majumbani huku alibainisha kuwa katika bajeti hiyo kipaumbele kikubwa ni sehemu ambayo wananchi hawapati huduma ya maji kabisa.

“Tumeanzisha utaratibu huu ili kuweza kuwaunganishia wananchi maaji hasa wale watakaohitaji, kitakachofanyika ni kutafuta mita na kuwafungia bure wao wataanza kulipia pale watakapoanza kutumia maji.”

Ameongeza kuwa wameomba shilingi bilioni 62.4 ili kuweza kukarabati, kuanzisha upya na kuendelea miradi mbalimbali ya maji Mkoani humo.

Kwaupande wao baadhi ya wenyeviti wa halmashauri wameipongeza RUWASA kwa Kasi waliyonayo ya kutekelezwa miradi ya maji kwenye maeneo yao Hali inayowapa wananchi imaani na serikali Yao.

Wameelezwa kuwa kikao hicho kumewapa mwanga wa kuweza kuwasilisha Maendeleo hayo kwa wananchi na kazi kubwa inayofanywa na serikali.

Kuhusu kuwafungia wananchi maji majumbani, wenyeviti hao wameipongeza hatua hiyo na kusema kuwa itasaidia kuondoa usumbufu kwa wananchi na itakuwa ni hatua moja wapo ya Maendeleo.

Aidha wameomba miradi iliyopo kwenye maeneo yao itekelezwe ambayo ilikuwepo tangu awali kabla ya kuanzishwa RUWASA huku ikiwa haitoi maji na kuwafanya wananchi wengine kulalamika huku wakimuomba katibu tawala mkoa kuzitaka taasisi nyingine Kama TANESCO na TARULA kuwa na vikao Kama walivyofanya RUWASA.

Akiongea kwenye kikao hicho kwaniaba ya Katibu tawala Mkoa wa Kagera Nesphory Bwana amewashukuru RUWASA kwa kuandaa mpango huo na kuwasilisha ukiwa unaonyesha namna walivyojipanga kumaliza tatizo la maji Kagera.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com