METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, July 23, 2020

TAWA YAZIDI KUWAVUTIA WATALII KUTEMBELEA MALIKALE ZA KILWA KISIWANI NA SONGO MNARA

vlcsnap-2020-07-23-13h57m37s538.pngEneo la Kivutio la Magofu ya Songo Mnara
vlcsnap-2020-07-23-13h58m53s193.png
Bi.Mercy Mbogelah Meneja Mhifadhi malikale katika Urithi wa utamaduni wa dunia magaofu ya Kilwa Kisiwani na Songo mnara chini ya Mamlaka ya Usimamizi ya wanyamapori Tanzania TAWA yaliyopo Wilayani Kilwa Mkoani LIndi akizungumzia vivutio vilivyopo katika maeneo hayo.
vlcsnap-2020-07-23-13h56m27s300.png
Moja wa Msikiti uliopo Kilwa Kisiwani ukiwa katika ubora ni eneo moja wapo la kivutio kwa watalii

JITIHADA  zinazofanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa  Wanyamapori Tanzania  TAWA katika kutangaza malikale katika Hifadhi ya Urithi wa utamaduni wa dunia Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara zinaendelea kuleta tija kwa Mamlaka hiyo kutokana na wageni wengi kufika katika Hifadhi hiyo ili kujionea vivutio hivyo.

Meneja Mhifadhi wa maeneo hayo  Bi. Mercy Mbogelah amesema kuwa hivi sasa kumekuwa na muitikio mzuri kwa wageni  kutoka ndani na nje ya nchi baada ya serikali kuruhusu shughuli za kitalii ambazo zilisimama kutokana na virusi vya Corona 
Akizungumza na wanahabari Bi Mbogelah ameeleza kuwa vivutio hivyo vilivyo katika Mji wa Kilwa Mkoani Lindi vina historia ya kipekee hapa nchini hasa ukizingatia kuwa ni Mji ambao ulikuwa ukitumia sarafu yake.

Ameeleza kuwa mji huo ambao ulijizolea umaarufu tangu karne ya 12 mpaka 16 ulikuwa ni kituo cha biashara ukanda wa Pwani ya Afrika Mashariki na mataifa mbalimbali kama Arabs,Indonesia,China,India na Ulaya ambapo walifika kufanya biashara na masultan waliokuwa wanaishi kilwa.

Sanjari na hayo Mji wa Kilwa ulikuwa chimbuko la  utamaduni wa Lugha ya Kiswahili,na Hivi leo kuna ushahidi wa majengo ya kale kama ngome ya mreno misikiti ya kale visima vya kale N.K

Baadhi ya wageni waliotembelea mali kale katika Hifadhi ya Urithi wa utamaduni wa dunia magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa  Wanyamapori Tanzania  TAWA kutoka nje nchi wamesema kuwa wameridhishwa na vivutio vilivyopo ndani ya eneo hilo na jitihada kubwa zinazofanywa na TAWA za kuboresha miundo mbinu zinazoendelea ndani ya Hifadhi ya Kilwa.

Mmoja wa wageni kutoka Nchini aliyetembea eneo hilo ni  Miss Utalii Mkoa wa Lindi 2020 Grace Mella amesema kuwa ameamua kutembelea eneo hilo kutokana na historia ya kipekee hapa nchini na yenye kusifika kwa kila pembe ya dunia.

Aidha Miss Utalii Lindi  ametoa wito hasa kwa jamii ya Kitanzania kuweza kutembelea eneo hilo kwa lengo la kujifunza historia mbalimbali za masultan katika Mji wa Kilwa Kisiwani na Songo Mnara.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com