Mara baada ya kukabidhiwa fomu na Katibu wa CCM wilaya ya Karagwe Mery Kananda, Bashungwa ametumia wasaa huo kumshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri nya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John P Magufuli kwa heshima aliyompatia yeye na wanakaragwe katika awamu hii ya miaka mitano kwa kumteua kuwa Naibu Waziri wa Kilimo na baadae kumteua kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.
Aidha, Amewashukuru wananchi wa wilaya ya karagwe kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi cha miaka mitano, maana asingeweza kutekeleza chochote bila ushirikiano wa wananchi wa karagwe na watanzania kwa ujumla.
Bashungwa amemaliza kwa kuwaomba wananchi wa wilaya ya karagwe waendelee kumuombea kwa safari hii ya mchakato wa uchaguzi ambao una changamoto na vikwazo mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment