Muonekano wa mradi wa Ujenzi wa Vihenge (8) unaotekelezwa Wilayani Babati Mkoani Manyara chini ya Wakala wa hifadhi ya chakula (NFRA)
Katibu mkuu Wizara ya Kilimo Bw Gerald Kusaya akitoka ndani ya moja ya Vihenge pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Kilimo alioambatananao katika ziara yake kujionea maendeleo ya maradi huo.
Katibu mkuu Wizara ya Kilimo Bw Gerald Kusaya akikagua nyumba za ofisi amabazo zitatumika na watendajiwa Wakala wa hifadhi ya chakula (NFRA) mradi huo utakapo kamilika.
Na Innocent Natai, Arusha
Katibu mkuu
Wizara ya Kilimo Bw Gerald Kusaya amewapongeza watendaji wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) na
mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa Vihenge (8) unaofanywa chini ya NFRA Wilayani Babati
Mkoani Manyara, kwa ajili ya uhifadhi wa nataka.
Ameyasema hayo alipotembelea katika eneo la ujenzi wa
Vihenge hivyo Babati Mkoani Manyara wakati wa kuhitimisha ziara yake ya kuzitembelea taasisi za Wizara ya Kilimo zilizopo Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro
na Manyara, lengo kuu likiwa ni kufahamiana na watumishi wa taasisisi hizo
pamoja na kupata taarifa za utendaji kazi wa taasisi hizo.
Akizungumzia ujenzi huo kusaya amesema kuwa mkandarasi wa
vihenge hivyo ameonyesha jitihadi kubwa katika kujali muda sambamba na ubora wa
vihenge hivyo pamoja na majengo.
“Mimi kama Katibu Mkuu wa Wizara hii ya Kilimo
nimetembelea mradi huu wa ujenzi wa vihenge pamoja na majengo, nimeridhishwa
na maendeleo ya ujenzi huu mkubwa wito wangu kwa mkandarasi wa ujenzi huu ni kuhakikisha unakamilishwa kwa wakati na ubora unaohitajika” alisema Kusaya
Kusaya ameongeza kuwa mradi huo wa ujenzi wa vihenge
utakapokamilika utakuwa na manufaa makubwa kwa taifa katika kuhakikisha kuwa
kunakuwepo na uhifadhi mkubwa wa chakula na pindi ambapo kutakuwa na uhaba wa
chakula kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) wataweza kusaidia
upatikanaji wa chakula kitakachokuwa kimehifadhiwa katika vihenge hivyo.
Aidha, kupitia wasaa huo aliwataka wataalam wa Wizara ya
Kilimo kuhakikisha wanatoa elimu ya uhifadhi bora wa mazao ya kilimo ili
kuwasaidia wakulima kuepukana na changamoto ya upotevu wa mazao baada ya mavuno
sambamba na “Sumukuvu”
MWISHO
0 comments:
Post a Comment