METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, March 19, 2020

HASUNGA AKIRI KUVUTIWA NA JITIHADA ZA TAHA KWENYE KUKUZA HORTICULTURE

Waziri wa kilimo Mhe.Japhet Hasunga akizungumza nawatendaji wa Taasisi ya kilimo cha horticulture TAHA, katika ofisi za makao makuu ya TAHA jijini Arusha. 

Mkurugenzi wa TAHA Dr.Jacqueline Mkindi akimkabidhi Waziri wa Kilimo Mhe.Japhet Hasunga(Mb) kofia na notebook za taasisi hiyo kama ishara ya kufika kwake kwenye taasisi hiyo jijini Arusha
Mkurugenzi wa TAHA Dr.Jacqueline Mkindi(katikati) akiwa na Meneja Mkuu wa Maendeleo wa shirika hilo Ndg.Anthony Chamanga(kushoto) pamoja na Waziri wa Kilimo Mhe.Japhet Hasunga(Mb)
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) (mwenye suti nyeusi) kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa TAHA makao makuu, alipofika kuwatembelea kwenye ofisi hizo.

Waziri wa kilimo Mhe.Japhet Hasunga amesema jitihada za asasi kilele ya kukuza na kuendeleza horticulture nchini TAHA kwenye kukuza tasnia ya horticulture ni dhahiri na zinastahili pongezi ya hali ya juu, huku akiifananisha taasisi na wizara ya kilimo kwa namna ilivyojipanga katika kutekeleza na kuendesha mambo yake.

Waziri hasunga ameyasema hayo katika ziara yake katika ofisi za makao makuu ya TAHA yalioko Arusha.

Akiwa na uso wenye furaha, Hasunga amesema TAHA imekipa tasnia ya horticulture hadhi stahiki kwani kwa sasa tasnia hiyo inatambulika na wizara imeanza kufanyia kazi kutokana na kwamba imeonyesha tija na kwa sababu TAHA imepaza sauti ya kutosha.

Mhe.Hasunga amebainisha kuwa kwa miaka yote wizara imekuwa ikitaja mazao 85 pekee yenye kuchangia kwenye pato jambo alilosema kuwa wamekuwa nyuma sana kutambua mara baada ya kujulishwa kuwa kwenye horticulture kuna Zaidi ya mazao 200.

Katika kuifanya sekta ndogo ya horticulture kuwa yenye tija Mhe. Hasunga amesema lazima kuwepo na mamlaka itakayoweza kusimamia sekta hiyo ili iwe yenye manufaa kwa nchi na wananchi wake.

“Natamani kabla ya kwenda kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, mamlaka ya kusimamia horticulture iwe imeanza kazi yake” alisema Mhe. Hasunga Mhe. Hasunga amesema pia licha ya TAHA kuonyesha kupendezwa na ushirikiano unaotolewa na serikali lakini yeye anaamini kuwa serikali ikiongeza nguvu Zaidi ya ushirika sekta hiyo itakuwa yenye tija Zaidi ya inavyoonekana
kwa sasa jambo ambalo amesema serikali itatekeleza.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com