Na innocent Natai, Morogoro
Mahakama
ya Wilaya ya Ifakara Mkoani Morogoro imemuhukumu kutumikia kifungo cha
mwaka mmoja jela au kulipa faini ya shilingi za kitanzania milioni mbili pamoja
na kulipa gharama za kuteketeza viuatilifu alivyo kamatwa navyo, Mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la,Yerusalem Mwamaja miaka 49 (Mhehe) baada ya
kupatikana na viuatiliafu ambavyo havijasajiliwa kinyume na kifungu cha
19 cha Sheria ya Hifadhi ya Mimea Na. 13 ya mwaka, 1997.
Hukumu
hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hio,Mheshimiwa Binge Njaga
Mashabara,baada ya kujiridhisha na hoja za mashahidi pamoja na vielelezo
vilivyo tolewa mahakamani na upande wa mashtaka,bila kuacha shaka yeyote.
Hakimu
Mashabara alisema vitendo kama hivyo vinawasababisha hasara kwa wakulima na
serikali kwa ujumla ukiachilia mbali kuendelea kusababisha madhara kwa
mazingira, afya za binadamu, wanyama na mimea. Hivyo alisema anatoa adhabu hiyo
ili iwe onyo na fundisho kwa wote wenye tabia kama hizo.
Awali,
mwendesha mashtaka,alidai kuwa hakukuwa na kumbukumbu za makosa ya nyuma dhidi
ya mshatakiwa huyo,sambamba na hilo na aliiomba Mahakama kutoa adhabu
kali ili iwe onyo na fundisho kwa wote wenye tabia kama hizo.
Katika
maombolezo yake Yerusalem Mwamaja alisema kuwa hakufahamu kama kufanya hivyo ni
kosa kisheria na aliomba apunguziwe adhabu kwani ni mara yake ya kwanza kufanya
kitendo hicho na hata rudia.
Akizungumzia
hukumu hio baada ya kutoka Mahakamani hapo Bw. Solomon Shedrack Mungure ambae
ni Mkaguzi wa Viuatilifu kutoka ofisi ya TPRI Dar es Saalam ametoa rai kwa
wauzaji na wasambazaji wa Viuatilifu nchi nzima wenye tabia za kuuza na
kusambaza viuatilifu ambavyo havija sajiliwa na kukaguliwa na TPRI kuacha mara
moja kwani zoezi la ukaguzi na kuwabaini watu kama hao ni endelevu hivyo
watakamatwa mara moja na kuwafikisha mahakamani.
Aidha
mkaguzi huyo amehitimisha kwa kusema kuwa kuuza au kusambaza viuatilifu bila
kuwa na elimu na kibali ni kosa kwani kunaweza kumsababisha madhara kwa
msambazaji,muuzaji au mtumiaji hivyo ni vyema kufuata taratibu za kupata kibali
ikiwemo kupata mafunzo yanayotolewa na TPRI ya matumizi sahihi na salama ya
viuatilifu.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment