Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na viongozi wa Chama cha Waajiri (ATE)
na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) walipokutana kwa lengo la
kujadili masuala mbalimbali ya Wafanyakazi na Waajiri, Novemba 2, 2019
Jijini Dodoma.
Sehemu ya viongozi wa Shirikisho
la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) wakifuatilia maelezo ya Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokutana nao Bungeni,
Jijini Dodoma. Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi
(TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe akifafanua
jambo wakati wa kikao hicho cha Utatu kilichowakutanisha kwa ajili ya
kujadili masuala mbalimbali ya Wafanyakazi na Waajiri.
Baadhi ya wajumbe kutoka Chama
cha Waajiri (ATE) na Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia majadiliano
wakati wa mkutano huo uliofanyika Jijini Dodoma.
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya akieleza jambo wakati wa mkutano huo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista
Mhagama akipitia taarifa wakati wa mkutano na viongozi wa Chama cha
Waajiri (ATE) na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA)
walipokutana kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya Wafanyakazi na
Waajiri, Jijini Dodoma.
Mkuu wa Huduma za Kisheria kutoka
Chama cha Waajiri (ATE) Bi. Suzan Ndomba akichangia mada wakati wa
mkutano huo uliofanyika Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya
Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe.
0 comments:
Post a Comment