Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi (Mb) akifungua Mkutano wa Kimataifa kuhusu Matumizi Bora ya Rasilimali za Ardhi katika Mandhari ya Afrika (African Landscapes Dialogue) unaofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha (AICC) jijini Arusha
Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bw. Fidelis Mutakyamilwa akimkaribisha Waziri kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) ambaye ndiye mwenyeji wa Mkutano huo Dkt. Stephen Nindi akitoa maelezo ya utangulizi kuhusu malengo na matarajio ya mkutano kabla ya kufuguliwa na Mh. Waziri
Mwakilishi wa Wizara ya Kilimo kutoka Serikali ya Uholanzi Bw. Hayo Haastra akitoa maelezo kwa washiriki namna Serikali ya Uholanzi inavyoshiriki kwenye mijadala ya matumzi ya ardhi katika mandhari mbalimbali za Afrika.
Mkurugenzi wa Eco Agriculture Sara Scherr, akitoa maelezo ya namna taasisi yake ilivyoshiriki katika maandalizi na kufanikisha kufanyika kwa Mkutano huo.
Mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) Boris Buechler akizungumza na washiriki kuhusu ushiriki wa Shirika hilo kwenye masuala mbalimbali ya matumizi ya rasilimali ardhi katika mandhari za Afrika
Mwakilishi kutoka Senegal Chimmere Diaw wa African Model Forest Network akiwasilisha mada ya jinsi ya kusimamamia mandhari jumuishi ya matumizi ya ardhi
Bwana John Recha kutoka programu ya mabadiliko ya Tabianchi akiwasilisha mada kuhusu upangaji matumizi ya ardhi katika mandhari mbalimbali kwa kuzingatia Sera na mabadiliko ya tabianchi
Mkurugenzi wa Shirika la Solidaridad Afrika Mashariki na kati Rachel Wanyoike, akiendesha moja ya mijadala kuhusu matumizi ya ardhi katika mandhari mbalimbali za Afrika
Washiriki wakifuatilia Mkutano
Picha ya pamoja ya washiriki wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu Matumizi Bora ya Rasilimali za Ardhi katika Mandhari ya Afrika (African Landscapes Dialogue)
(Picha na Fredy Njeje)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi, amefungua Mkutano wa Kimataifa kuhusu matumizi bora ya rasilimali ardhi kwenye
Mandhari mbalimbali za Afrika wenye lengo la kujadili hali halisi na kubadilishana uzoefu
katika upangaji, utekelezaji na usimamizi wa mipango ya matumizi ya ardhi
katika Mandhari hizo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo Mh. Lukuvi amewapongeza Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) kama
muandaaji mwenyeji, Asasi zisizo za Kiserikali za Eco Agriculture Partners pamoja na wadau wengine wote
waliofanikisha kufanyika kwa mkutano huo na Tanzania kuwa mwenyeji kwa mwaka
huu.
Aidha, Mh. Lukuvi amewataka wadau
hao kutoka ndani na nje ya nchi kushirikiana na kubadilishana uzoefu katika
utekelezaji wa masuala mbalimbali ya kisekta yenye lengo la kuimarisha Mandhari
Duniani hasa katika kipindi hiki ambacho mabadiliko ya tabia nchi yanazidi
kushamiri na kuathiri uzalishaji na maisha ya binadamu katika maeneo mbalimbali
Duniani.
Mkutano huo wa siku nne,
unatarajiwa kujadili masuala ya uanzishwaji na utawala wa mandhari, utekelezaji
na upangaji wa mandhari kwa kuzingatia mabadiliko ya tabianchi, uimarishaji wa
biashara, ajira na ujasiriamali katika uchumi wa kijani. Masuala mengine ambayo
yanatarajiwa kujadiliwa ni pamoja na usimamizi wa wanyamapori na bionuai katika
mandhari pamoja na udhamini kifedha, Uwekezaji, haki za miliki na matumizi ya
ardhi katika mandhari.
Inategemewa kuwa, kufanikiwa kwa
utekelezaji wa masuala hayo yote katika nchi mbalimbali za Afrika na dunia kwa
ujumla itakuwa ni chachu katika kuimarisha uchumi na kuleta maendeleo ya nchi
na hatimaye kufanikiwa kwa malengo endelevu ya maendeleo (Sustainable
Development Goals)
0 comments:
Post a Comment