Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe
akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa
Afrika – Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic
katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Waziri wa mambo ya nje wa Norway Ine Marie Eriksen Sereide
akizungumza katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika –
Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika
Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.
Palamagamba Kabudi akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Mawaziri wa
Mambo ya Nje wa Afrika – Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi
za 5 za Nordic katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini
Dar es Salaam.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza na Waziri Mkuu
Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba wakati wa Mkutano wa Mawaziri wa Mambo
ya Nje wa Afrika – Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5
za Nordic katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es
Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara,
Philip Mangula katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika –
Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika
Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka nchi mbalimbali wakiwa
katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika – Nordic
unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo cha
Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira
Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja (wa Kwanza kukulia)
akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL),
Waziri Kindamba (wa Pili toka kulia) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika – Nordic unaoshirikisha nchi 29 za
Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano
(JNICC) jijini Dar es Salaam. .
Baadhi ya Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka nchi mbalimbali wakiwa
katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika – Nordic
unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo cha
Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam.
Washiriki katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika –
Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika
Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es salaam.
Balozi wa China nchi Wang Ke akizungumza na Naibu Waziri wa
Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumaro
katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika – Nordic
unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo
cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Waziri wa mambo ya nje wa Norway Ine Marie Eriksen Sereide
akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira, Mh. George Simbachawene katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo
ya Nje wa Afrika – Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5
za Nordic katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es
Salaam.
Washiriki katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika –
Nordic unaoshirikisha nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika
Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda akisalimiana na
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima nchini Josephat Gwajima katika
Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika – Nordic unaoshirikisha
nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo cha Kimataifa cha
Mikutano (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali baada ya kuifungua
Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika – Nordic unaoshirikisha
nchi 29 za Afrika na nchi za 5 za Nordic katika Kituo cha Kimataifa cha
Mikutano (JNICC) jijini Dar es Salaam.
...................
Na Mwandishi Wetu.
Afrika haitaweza kupiga hatua endapo itaendelea kuwa muuzaji wa bidhaa ghafi na muagizaji wa bidhaa za viwandani.
Kauli hiyo imetolewa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Joseph Magufuli wakati wa ufunguzi
wa mkutano wa Mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi za Afrika na Nordic
unaofanyika jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli amesema kuwa kwa
sasa, asilimia 60 ya mauzo ya nje kutoka nchi za Afrika ni mazao ghafi
hivyo ni lazima Waafrika tufike hatua ambapo tutaweza kusindika na
kuongeza thamani ya mazao yetu, ikiwemo mazao ya kilimo, madini, uvuvi,
nk.
“Tunataka tusindike pamba na
kutengeneza nguo hapa Afrika; tunataka tuchimbe madini na kuyachenjua
hapa hapa Afrika; tunataka tuvue samaki na kuwasindika hapa hapa Afrika.
Africa must produce, process, consume and export finished products,”
amesema.
Ameongeza kuwa Viwanda ni moja ya
vipaumbele vyetu vikubwa, na washirika wetu wa maendeleo pamoja na
wawekezaji wengine makini watuunge mkono kwenye mwelekeo huo.
Amesema kwa kuwa nchi marafiki za
Nordic wamepiga hatua kiteknolojia, hususan teknolojia ya viwanda,
tushirikiane kujenga viwanda vya kusindika na kuongeza thamani ya mazao
yetu kwa manufaa ya pande zetu mbili.
Vile vile ameosema ili kuweza ili
kuvutia biashara na uwekezaji katika sekta mbalimbali, ni muhimu kwa
nchi za Afrika kuweka mazingira muafaka, ikiwemo miundombinu wezeshi
pamoja na kuondoa urasimu kwenye sheria na taratibu zetu za biashara na
uwekezaji.
Amesema mpaka sasa Tanzania
imefanikiwa kupitia na kurekebisha sheria na taratibu mbalimbali za
uwekezaji nchini, ikiwa ni pamoja na kutengeneza sheria za kuwalinda
wawekezaji.
“Tumeanzisha Wizara mahsusi yenye
dhamana ya Uwekezaji chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ili ijihusishe moja
kwa moja na kurahisisha mazingira na uratibu wa uwekezaji nchini,”
amesema.
Lakini muhimu zaidi, tunatekeleza
Mkakati wa Kurekebisha na Kuboresha Mazingira ya Biashara nchini, yaani
The Blueprint for Regulatory Reforms to Improve Business Environment.
Jitihada zingine ni kutenga kanda maalum kwa ajili ya ujenzi wa viwanda
na kanda maalumu za uwekezaji, yaani Export Processing Zones and Special
Economic Zones.
Sambamba na hayo, Tanzania
kutambua umuhimu wa miundombinu wezeshi kama kichocheo cha biashara na
uwekezaji, hivi sasa, inajenga na kuboresha miundombinu ya usafiri na
usafirishaji, ikiwemo barabara, reli, usafiri wa majini na anga.
Amesema hivi sasa wanajenga Reli
ya Kisasa, yaani Standard Gauge Railway kwenye Ushoroba wa Kati yenye
urefu wa kilomita 1,800 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, ambayo baadaye
itaunganisha na nchi jirani za Rwanda na Burundi.
Ameongeza kuwa ili kuvutia
wawekezaji wameza kulifufua Shirika letu la Ndege la ATCL na kuboresha
viwanja vyetu vya ndege na kusimika rada za kuongozea ndege. Tunapanua
na kuboresha bandari zetu za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga pamoja
zilizopo kwenye Maziwa yetu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa.
Na upanuzi huu umeenda sambamba na
ujenzi wa meli na vivuko. Zaidi ya hapo, tutakeleza Mradi mkubwa wa
uzalishaji wa umeme wa maji kwenye Bonde la Rufiji utakaozalisha
Megawati 2,115, na kuchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za
uzalishaji wa bidhaa viwandani na kwenye sekta nyingine.
Amemalizia kwa kuzikaribisha nchi
za Nordic, pamoja na mataifa mengine, yakiwemo ya Afrika, kuja kuwekeza
nchini Tanzania ambapo kuna mazingira wezeshi ya uwekezaji ni muafaka na
yanatabirika, kutokana na amani na utulivu wa kisiasa, lakini pia
mwenendo wa ukuaji wa uchumi ni mzuri ambapo, kwa sasa, ni wastani wa
asilimia 7. Zaidi ya hapo, Tanzania ni wanachama wa SADC na EAC, ambazo
kwa pamoja zina idadi ya watu wapatao milioni 450.
0 comments:
Post a Comment