Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),Mhe.Mwita Waitara, akizungumza
wakati wa maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani, yaliyoenda
sambamba na uzinduzi wa Ripoti ya Idadi ya watu Duniani, tukio
lililofanyika jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Mkazi wa Umoja wa
Mataifa(UN), Alvaro Rodriguez,akitoa taarifa wa maadhimisho ya siku ya
idadi ya watu duniani, yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Ripoti ya
Idadi ya watu Duniani, tukio lililofanyika jijini Dodoma.
Muwakilishi wa Shirika la UNFPA nchin Tanzania Bi.Jacqueline Mahon,akitoa ripoti ya idadi ya watu duniani iliyotolewa na Shirika hilowakati
wa maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani, yaliyoenda sambamba
na uzinduzi wa Ripoti ya Idadi ya watu Duniani, tukio lililofanyika
jijini Dodoma.
Afisa kutoka UNFPA,Bw.Samwel Msokwa,
akisoma taarifa ya idadi ya watu duniani iliyotolewa na Shirika
hilo wakati wa maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani, yaliyoenda
sambamba na uzinduzi wa Ripoti ya Idadi ya watu Duniani, tukio
lililofanyika jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe.Patrobas
Katambi akizungumza katika maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani,
yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Ripoti ya Idadi ya watu Duniani,
tukio lililofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya wadau wakifuatilia maadhimisho
ya siku ya idadi ya watu duniani, yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa
Ripoti ya Idadi ya watu Duniani, tukio lililofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),Mwita Waitara, akizindua Ripoti ya
Idadi ya watu Duniani,kushoto kwake ni Mwakilishi wa Mkazi wa Umoja wa
Mataifa(UN), Alvaro Rodriguez,wa pili ni Mkuu wa wilaya ya Dodoma
Mhe.Patrobas Katambi na kulia ni Muwakilishi wa Shirika la UNFPA nchin
Tanzania Bi.Jacqueline Mahon,tukio lililofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),Mwita Waitara,akiwa katika picha ya
pamoja na meza kuu baada ya kuzindua Ripoti ya Idadi ya watu
Duniani,Kulia ni Muwakilishi wa Shirika la UNFPA nchin Tanzania Bi.Jacqueline Mahon,akifuatiwa
na Mwakilishi wa Mkazi wa Umoja wa Mataifa(UN), Alvaro Rodriguez,na
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mhe.Patrobas Katambi wakiwa wameshika ripoti
hiyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),Mwita Waitara,akiwa amenyanyua
vitabu mara baada ya kuzindua Ripoti ya Idadi ya watu Duniani,uzinduzi
huo ulifanyika jijini Dodoma.
………………
Na Alex Sonna, Dodoma.
LICHA ya Serikali kuweka adhabu kali
dhidi ya watu wanaowasababishia ujauzito wanafunzi na watoto waliochini
ya umri wa miaka 18, lakini bado tatizo la mimba za utotoni ni kubwa
huku mila na desturi zikitajwa kuchangia tatizo hilo hapa nchini
Tanzania.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),Mwita Waitara,
wakati maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani, yaliyoenda
sambamba na uzinduzi wa Ripoti ya Idadi ya watu Duniani, tukio
lililofanyika jijini Dodoma.
Mhe. Waitara amesema tatizo hilo ni kubwa
kwa shule za msingi na sekondari ambapo ni asilimia 29 na linachangiwa
kwa kiasi kikubwa na mila na desturi, uendeshaji wa kesi ya kumtia mtu
hatiani aliyempa mimba wanafunzi.
“Kuna mila na desturi ambazo watoto wa
kike wakifikia umri fulani wanapewa chumba hivyo huko mtaani usiku kucha
huwezi jua kinachoendelea, mazingira magumu ya usomaji.
“Hata katika uendeshaji kesi hizi mpaka
kumtia mtu hatiani bado ni changamoto sana kwa kuwa wanaofanya vitendo
hivyo wengine ni watu wa karibu na familia na wengine wanarubuni ndugu
na kumalizana kimya kimya,”amesema Waitara.
Aidha licha ya hayo amesema uelewa wa
watoto bado ni mdogo huku mimba nyingi zinaripotiwa lakini zinaishia
hewani bila kujua mwisho wa kesi hiyo.
Amesema wao kama serikali wanafanya vikao
na wazazi mara kwa mara ili kuondokana na tatizo hili, lakini bado
mwitikio ni mdogo sana katika kudhibiti vitendo hivi.
Kadhalika, amesema bado kuna changamoto
ya vifo vitokanavyo na uzazi ambapo kati ya vizazi hai 100,000 watu 556
huripotiwa kufariki dunia kwa sababu mbalimbali ikiwemo mimba za utoto.
“Nchi yetu ni moja ya mataifa 179
yaliyokutana nchini Cairo na tulikubaliana kutekeleza Mpango kazi
tuliopanga wa katika Mkutano huo wa Idadi ya watu na maendeleo, serikali
ya Tanzania imetekeleza mambo mengi, ni wajibu wetu kushirikiana
kumaliza vifo vinavyotokana uzazi na mimba za utotoni ili kila kijana
atimize ndoto zake,”amesema.
Pia amebainisha kuwa serikali imekuwa
ikitekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo na inalenga kufikia uchumi
wa kati ifikapo mwaka 2025.
Kwa upande wake afisa kutoka UNFPA,
Samwel Msokwa, akisoma taarifa ya idadi ya watu duniani iliyotolewa na
Shirika hilo, amesema kadri watu wanavyoongezeka changamoto nazo
zinaongezeka ambapo katika ripoti hiyo inaonesha tatizo la mimba za
utotoni duniani bado ni kubwa sana.
Ambalo mara kwa mara linaathiri mipango
mbalimbali ya vijana wengi wanahitaji kupata fursa, au kujiendeleza
zaidi katika elimu, huku vifo vya akina mama wajawazito navyo
vikiongezeka.
“Ripoti inaeleza kinaga ubaga kuwa kuna
tatizo la ukatili wa kijinsia licha ya taasisi mbalimbali kufanyiwa
kazi, tuelekeze nguvu kukabiliana na tatizo hili,”amesema.
Naye, Mwakilishi wa Mkazi wa Umoja wa
Mataifa(UN), Alvaro Rodriguez amesema vifo vinavyotokana na uzazi bado
ni changamoto hasa kwa wasichana wenye umri kati ya miaka 15-19.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Damas Ndumbaro ( wa pili kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Kilabu hiyo Antonio Sanches ( wa kwanza kush...
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akishiriki zoezi la upandaji wa mbegu za pamba kwenye shamba la watumishi wa halmashauri ya mji wa Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita,akiwasili kwenye eneo la shamba na kusalimiana na viongozi wa halmashauri hiyo akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi.
Afisa Kilimo wa halmashauri ya mji,Bw Samwel Ng'wandu akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita pamoja na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita,Leornad Kiganga.
Baadhi ya watumishi na Jeshi la akiba (MGAMBO)wakishiriki shughuli za kupanda mbegu kwenye shamba la watumishi wa halmashauri ya mji.
NA JOEL MADUKA,GEITA
Wataalamu wa kilimo mkoani Geita wametakiwa kuwafuatilia kwa karibu wakulima wa pamba na kuwaelekeza kulima kwa tija ili kuzalisha zaidi tofauti na miaka ya nyuma.
Akizindua msimu wa kilimo cha pamba kwenye mashamba ya watumishi wa Halmashauri ya mji wa Geita yaliyoko kata ya Buhalahala ,Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi alisema ni vema wataalam hao wakafika kwenye maeneo ya kilimo na kuwaelekeza wakulima kanuni zitakazowasaidia kuvuna pamba nyingi.
“Wito wangu kwa wakulima wote pamoja na wataalam wetu wa kilimo baada ya uzinduzi huu mkubwa kabisa wa kilimo cha pamba Mkoani kwetu,wataalam ni vyema wakawasaidia wakulima kufuata zile kanuni kumi bora za kilimo ambacho kitaweza kuwa saidia wakulima lakini nataka twende kisayansi zaidi”Alisema Luhumbi.
Mhandisi Luhumbi Aliongezea Kuwa Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kumsaidia mkulima na kuwataka wakulima kuchangamkia fursa hiyo na kuwekeza katika sekta ya kilimo cha pamba kwa kuwa hali ya hewa ya mwaka huu ni nzuri.
Mshahuri wa kilimo cha Mkataba Mkoani Geita Bw Joshua Mirumbe alisema lengo ni kuhakikisha wanaongeza tija ya uzalishaji kutoka wastani wa kilo 250 hadi 300 na kwenda kwa wastani wa kilo 800.
Katika msimu wa mwaka 2016/2017 mkoa wa Geita ulilenga kulima hekta 67002 zilizotarajiwa kuzalisha tani ,93437 za pamba lakini utekelezaji ulikuwa hekta 24 791 zilizozalisha tani 13 267.8 zenye thamani ya Sh Bilioni 15.
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akishiriki zoezi la upandaji wa mbegu za pamba kwenye shamba la watumishi wa halmashauri ya ...
0 comments:
Post a Comment