WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema
Serikali ya Kenya imesema kauli iliyotolewa na Mbunge wa jimbo la
Starehe nchini humo, Charles Njagua Kanyi maarufu Jaguar si kauli ya
Serikali, hivyo amewataka Watanzania wawe watulivu.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo
(Jumanne, Juni 25, 2019) wakati akitoa kauli ya Serikali kuhusu kauli ya
iliyotolewa na mbunge huyo ya kuwataka wafanyabiashara kutoka nchi
mbalimbali ikiwemo Tanzania waondoke nchini Kenya ndani ya saa 24.
Amesema baada ya mbunge huyo kutoa kauli
hiyo, Serikali ilianza kulifanyiakazi jambo hilo ambapo ilimuita Balozi
wa Kenya nchini Tanzania ili kujua kama huo ni msimamo wa Serikali yao
ama la, ambapo balozi huyo alimesema ile si kauli ya Serikali ya Kenya
wala wananchi.
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema mbali na
kuwasiliana na Balozi huyo, pia Serikali imewasiliana na Balozi wa
Tanzania nchini Kenya ili afuatilie kuhusu kauli ya Mbunge huyo, hivyo
amewataka Watanzania waendelee kushirikiana na Wakenya.
“Si kauli nzuri na kauli hii iliyotolewa
na mtu mmoja linajenga chuki baina ya mtu na mtu, nchi na nchi na tayari
Serikali ya Kenya inalifanyia kazi suala hili na imetuomba Watanzania
tuendelee kuwa wavumilivu.”
Waziri Mkuu amesema tamko lile linaweza
kuibua chuki na vurugu miongoni mwa nchi mbalimbali zikiwemo za Afrika
Mashariki na tayari Wabunge wa Bunge Afrika Mashariki wanaoendelea na
kikao cha Bunge hilo jijini Arusha wamepinga na kulaani kauli hiyo.
Wamesema hawatoa nafasi kwa mtu yeyote kuvuruga nchi hizo.
Hivyo, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo
kuwasihi Watanzania popote walipo waendelee kuishi vizuri na Wakenya kwa
kuwa wao hawana chuki na Watanzania bali ni mtu binafsi. Pia
amewatahadharisha wananchi wa Afrika Mashariki wawe makini na kauli zao
ili kuepusha vurugu.
0 comments:
Post a Comment