Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba Tuzo ya Uwezeshaji Kiuchumi, baada ya
Wizara ya kilimo kuibuka mshindi wa pili katika kundi la Wizara, Wakala na Idara za
Serikali kwenye Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
lililofunguliwa na Waziri Mkuu katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma Juni 18,
2018. (Picha Na Mathias Canal Wizara ya Kilimo)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha Taarifa ya Utekelezaji
wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya Mei 2017 Mpaka Mei 2018
baada ya kuizindua katika Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi lililofanyika kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. Kushoto
ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. John Jingu.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua
Kongamano hilo kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na baadhi ya viongozi
walioshiriki katika Ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi wakipiga makofi baada ya Waziri Mkuu kufungua Kongamano hilo kwenye
ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma Juni 18, 2018. kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi
ya Waziri Mkuu Profesa, Faustine Kamuzora,
Meya wa jiji la Dodoma Profesa Davis Mwamfupe, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe
Anthony Mtaka, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Dkt. John
Jingu, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dkt.
Binilith Mahenge na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi, Beng'i Issa.
Na Mathias Canal-WK,
Dodoma
Wizara ya kilimo imeipuka Wizara ya
Maliasili na Utalii kwa kuwa wizara iliyoshika nafasi ya pili kama wizara
iliyofanya vizuri dhidi ya taasisi nyingine za serikali zikiwemo wizara katika utekelezaji
wa shughuli na programu mbalimbali za uwezeshaji wananchi kiuchumi, kuongeza
ujuzi na kuimarisha uratibu wa shughuli za uwezeshaji katika kipindi cha mwaka
2017/2018.
Kwa niaba ya wizara ya kilimo tuzo hiyo imepokelewa na Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba ambaye amesema
kuwa wizara yake ilistahili kushika nafasi ya kwanza kwani imefanya majukumu
makubwa kupitia nafasi yake ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Tuzo hiyo dhidi ya Wizara zilizofanya vizuri, Taasisi za serikali, na wajasiriamali
zimetolewa leo (Jumatatu, Juni 18, 2018) na waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano
wa Tanzania Kassim Majaliwa wakati
akifungua Kongamano la Tatu la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
LAPF, Jijini Dodoma.
Katika hafla hiyo WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema taarifa ya Kongamano la Uchumi la Dunia la mwaka 2018 inaonesha
kuwa Tanzania inaongoza kwa kuwa na uchumi jumuishi miongoni mwa nchi za Afrika
zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Amesema hali hiyo, imetokana na Tanzania kufungua fursa za
ujasiriamali ambapo kuna zaidi ya biashara milioni tatu zinazokuwepo kila
mwaka, lengo la nchi ni kuhakikisha kuwa uchumi unakua na unamgusa kila
Mtanzania hususan mwananchi wa kawaida.
Waziri Mkuu ameongeza kwamba Serikali inaamini
kuwa uchumi wa viwanda ukiimarika uchumi utakuwa kwa kasi kubwa na matokeo yake
yataonekana wazi kwa kupanua wigo wa ajira, soko la huduma na shughuli nyingine
za kiuchumi.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema suala la uchumi wa viwanda kuelekea uchumi
wa kati ifikapo mwaka 2025 ni moja ya ajenda muhimu ya Serikali ya Awamu ya
Tano, hivyo amezitaka sekta zote zihakikishe zinatoa mchango mkubwa kwenye
uchumi wa viwanda.
Wakala wa barabara nchini ndio umeongoza kwa kushika nafasi ya
kwanza iliyofanya vizuri dhidi ya taasisi nyingine za serikali huku vigezi
vilivyotumika kuwapata washindi ikiwa ni pamoja na kutengeneza mazingira
wezeshi kwa watanzania kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi katika
mwaka wa fedha 2017/2018 kwa mabadiliko ya sera, sheria, kutengeneza kanuni,
mikataba, kujenga uwezo n.k
Kongamano hilo lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi (NEEC) limehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista
Mhagama, Waziri wa Kilimo Dkt Charles Tizeba, Waziri Viwanda, Biashara na
Uwekezaji Bw. Charles Mwijage na Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Bw. Suleiman Jafo.
Wengine ni Wakuu wa Mikoa mbalimbali, Makatibu Wakuu wa
Wizara, Wakuu wa Wilaya ya Mkoa wa Dodoma, Makatibu Tawala wa Mikoa,
Mwenyekiti na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi,Wakurugenzi wa Halmashauri za Mamlaka za Serikali za Mitaa,
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
Bibi Beng’ Issa, wadhamini wa Kongamano hilo na Wawakilishi kutoka katika
taasisi mbalimbali za Serikali na Sekta binafsi.
0 comments:
Post a Comment