Mbunge
wa jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete ,akizungumza wakati wa uzinduzi
wa madarasa sita na ofisi moja ya walimu katika shule ya msingi Pakistan
utete kata ya Pera,yaliyokarabatiwa kwa ufadhili wa marafiki wa
Pakistan.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete kushoto akiagana na balozi wa
Pakistan nchini Amir Khan baada ya kuzindua majengo ya madarasa sita na
ofisi moja ya walimu katika shule ya msingi Pakistan utete kata ya
Pera,yaliyokarabatiwa kwa ufadhili wa marafiki wa Pakistan.(Picha na
Mwamvua Mwinyi)
Balozi
wa Pakistan nchini,Amir khan wa kushoto na mbunge wa jimbo la Chalinze
Ridhiwan Kikwete,wakizindua majengo ya madarasa sita na ofisi moja ya
walimu katika shule ya msingi Pakistan utete kata ya
Pera,yaliyokarabatiwa kwa ufadhili wa marafiki wa Pakistan.(Picha na
Mwamvua Mwinyi)
Balozi wa Pakistan nchini,Amir
khan wa kushoto na mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwan
Kikwete,wakikagua majengo ya madarasa sita na ofisi moja ya walimu
katika shule ya msingi Pakistan utete kata ya Pera,yaliyokarabatiwa kwa
ufadhili wa marafiki wa Pakistan.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Balozi wa Pakistan nchini,Amir
khan wa kushoto na mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwan
Kikwete,wakiingia katika lango kuu la majengo ya madarasa sita na ofisi
moja ya walimu katika shule ya msingi Pakistan utete kata ya
Pera,yaliyokarabatiwa kwa ufadhili wa marafiki wa Pakistan.(Picha na
Mwamvua Mwinyi)
Balozi
wa Pakistan nchini Tanzania,Amir Khan akizungumza baada ya kuzindua
majengo ya madarasa sita na ofisi moja ya walimu yaliyokarabatiwa na
marafiki wa Pakistan katika shule ya msingi Pakistan utete iliyopo kata
ya Pera,kushoto kwake ni mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwan
Kikwete.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
MBUNGE
wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete,amewahimiza wananchi kujenga
tabia ya kujitolea katika shughuli za kimaendeleo pasipo kuachia
serikali/halmashauri na wahisani pekee.
Aidha
amesema ofisi yake na halmashauri wataendelea kuunga mkono juhudi za
wafadhili na wadau wanaojitokeza kushirikiana nao kutatua changamoto
zinazowakabili jimboni hapo ikiwemo elimu.
Ridhiwani
alitoa rai hiyo, wakati wa uzinduzi wa majengo ya madarasa sita na
ofisi moja ya walimu katika shule ya msingi Pakistan Utete iliyopo kata
ya Pera,Chalinze wilayani Bagamoyo,yaliyokarabatiwa kwa ufadhili wa
marafiki wa Pakistan,kwa gharama ya sh.milioni.30.
Alisema baadhi ya wafadhili wanasaidia endapo wanaona jamii husika ikichukua juhudi na kufikia hatua mbalimbali .
Aliwataka
wananchi wa Chalinze kushirikiana na serikali,halmashauri na wafadhili
wanaojitokeza ili kukamilisha miradi ya maendeleo iliyopo kwenye maeneo
yao.
“Ajenda kubwa tuliyonayo ni kuboresha na kutatua changamoto katika sekta ya elimu”
“Pamoja
na shughuli zinazofanywa na wahisani lakini haina budi wananchi
mkajitolea katika shughuli za maendeleo ili tukienda kuomba msaada kwa
wafadhili waweze kukubali kirahisi kwa kuona hatua ambazo zimeanza
kuchukuliwa “alisema Ridhiwani.
Ridhiwani
alisema wakati marafiki wa Pakistan wakiwezesha ukarabati huo,lakini
halmashauri ya Chalinze imeshatenga fedha kwa ajili ya kujenga matundu
ya vyoo nane katika shule ya Pakistan Utete.
Hata
hivyo,mbunge huyo alieleza kwamba,pia wanajenga matundu ya vyoo katika
shule ya msingi Mbala sanjali na madarasa mawili ya shule ya msingi
Makombe.
Ridhiwani
alieleza,ujenzi wa matundu ya vyoo utasaidia kuondoa kero ya uchafu wa
mazingira ambapo baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakijisaidia ovyo maporini
,vichakani .
“Kwasasa kilichobakia ni usimamizi katika hatua ya ujenzi unaoendelea kwenye shule hizo ”alisema Ridhiwani.
Akizungumzia msaada walioupata kutoka kwa marafiki wa Pakistan,Ridhiwani aliomba ushirikiano ulioonyeshwa usiishie hapo .
Alimpongeza mwenyekiti wa kitongoji Hussein Mramba na diwani wa kata ya Pera kwa jitihada walizozichukua kusukuma jambo hilo.
Ridhiwani
hakusita kumuomba balozi wa Pakistan nchini Tanzania,Amir Khan
,kuwasaidia ujenzi wa jengo la kulaza wagonjwa na mashine za kupima
magonjwa katika kituo cha afya Chalinze.
Akizindua
majengo hayo,balozi wa Pakistan nchini Khan,alisema amefurahishwa na
ushirikiano uliopo baina ya nchi hiyo na Tanzania,na alishauri kuwepo na
mahusiano kati ya wabunge wa Pakistan na Tanzania.
“Nilipoambiwa
kuja shuleni hapa ni km 120 kutoka Dar es salaam nikaona nije kutembea
na kuona kilichofanyika,Nawapongeza kwa kuanzisha ujenzi huu ili watoto
wapate elimu”alisema Khan.
Alisema
ili watoto hao wasome vizuri ni vyema kukajengwa uzio katika shule hiyo
ili kuweka usalama zaidi hivyo wanatasaidia kuujenga.
Balozi
huyo,aliahidi na kukubali ombi la kusaidia mashine na vifaa vya kituo
hicho cha afya lakini kwasasa wanachotakiwa kufanya ni kuandika maombi
ya msaada huo.
0 comments:
Post a Comment