METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, August 9, 2017

NACHINGWEA YASHIKA NAFASI YA TATU MAONESHO YA NANENANE KITAIFA 2017

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimshukuru Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Mhe Rukia Muwango kwa zawadi mbalimbali wakati alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea kabla ya kufunga maadhimisho ya sikukuu ya wakulima, (Nane nane) ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017. 
 
Na Mathias Canal, Lindi

Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi imeshika nafasi ya tatu katika maonyesho ya nane nane ambayo huhusisha maswala ya Kilimo Mifugo na Uvuvi yaliyofanyikia Jijini Mbeya kwa kanda ya kusini na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali.

Akizungumza mara baada ya kupokea zawadi ya kuwa washidi wa tatu wa maonyesho hayo ya nanenane  Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe Rukia Muwango aliwapongeza wananchi na viongozi wa wilaya hiyo kwa kufanya vizuri katika maonyesho hayo kwa kile walichokifanya na kuonyesha kuwa Wila ya Nachingwea sekta ya Kilimo inasaidia kuinua kipato kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

"Mimi niwashukuru sana kwa zawadi waliyotupa wananchi na viongozi wa Wilaya ya Nachingwea maana ushindani ulikuwa mkubwa mno hasa ukiangalia wilaya zote za kanda ya kusini zinasifika sana kwa Kilimo cha mazao mbalimbali na ufugaji hivyo haikuwa rahisi sana kufika hapa mwaka huu" Alisema Muwango

Muwango alisema kuwa atakaa na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Kupanga mikakati madhubuti ili mwakani waweze kushika nafasi ya kwanza na kuwa wilaya ya mfano.

Aidha, Muwango alisema mikakati yake ni kuboresha pale walipokwama ili kupata matokeo chanya katika maonyesho yajayo.

"Mikakati iliyopo ni kwamba mwisho wa maonesho haya ndiyo mwanzo wa maonesho mengine, tumegundua vitu vilivyotufanya kuwa namba tatu ni pamoja na ubunifu, hivyo tutazidi kuwa wabunifu kwa maonesho yajayo ili tufikie ushindi mnono zaidi" alisema Muwango
 
Katika Maonesho hayo nafasi ya pili imechukuliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Lindi huku nafasi ya kwanza ikinyakwa na Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.
Katika maadhimisho hayo ya Nanenane 2017 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan alisisitiza zaidi wananchi katika mkoa wa Lindi na Mtwara kutumia pesa walizopata wakati wa mavuno kujenga makazi bora, kusomesha watoto na kununua chakula cha kutosha familia zao.

Aidha aliwasifia wakulima hao kwa namna ambavyo wameweza kupokea  teknolojia za kilimo hivyo kubadilisha sura ya maonesho ikilinganishwa na maonesho ya mwaka jana.

MWISHO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com