Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro amewataka Makamishna
wastaafu kuendeleza elimu ya polisi jamii pamoja na kutoa msaada wowote
utakaohitajika kwa jeshi la hilo.
Ameyasema
hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe za kuwaaga
makamishna wastaafu zilizofanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa
Polisi kilichopo jijini humo.
Aidha,
Makamishna walioagwa ni pamoja na Paul Chagonja, Hamdan Omar Makame na
Kenneth Kaseke, ambapo amesema kuwa kazi waliyofanya wastaafu hao ni
kubwa lakini kustaafu kwao sio mwisho wa kutumika katika jeshi la
polisi.
“Upolisi
ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine hivyo utaalamu hauzeeki na
kwetu sisi tunaondelea kubaki Jeshini tutaendelea kufuata yale yote
mazuri mliyofanya na nyie mnapokuwa nje ya utumishi endeleeni kutusaidia
kwa mawazo na milango yetu ipo wazi ili kuhakikisha nchi inaendelea
kuwa salama,” amesema IGP Sirro
Kwa
upande wake, Paul Chagonja ambaye alikuwa Kamishna wa Oparesheni na
mafunzo kwa muda mrefu amewaasa Maofisa na Askari kuendeleza tamaduni na
maadili ya Polisi pamoja na kufanya kazi kwa weledi.
Sherehe
hizo zimehudhuriwa na Viongozi mbalimbali kutoka vyombo vya ulinzi na
usalama, Mkurugenzi wa Takukuru Kamishna, Valentino Mlowola, IGP Mstaafu
Said Mwema, DCI Mstaafu, Robert Manumba na Kamishna Mstaafu wa Kanda
Maalumu ya Dar Es Salaam, Suleiman Kova pamoja na maofisa na Askari
Polisi.
0 comments:
Post a Comment