Wakati wanachama 100 wamejitokeza kuwania
nafasi mbalimbali za uongozi kuwakilisha mkoa huo, wanachama 331 wamejitokeza
kuwania nafasi hizo katika wilaya nne za kichama za mkoa wa Iringa, Mufindi,
Kilolo, Iringa Vijijini na Iringa Manispaa.
Akizungumza na wanahabari leo Jumatano, Katibu wa
CCM Mkoa wa Iringa, Christopher Magala alisema wagombea 13 wamejitokeza kuwania
nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa huku 12 wakiwania nafasi ya ujumbe wa halmashauri
kuu ya Taifa na 15 nafasi ya Katibu wa Itikadi Siasa na Uenezi mkoa.
Waliojitokeza kuwania nafasi ya
mwenyekiti ni pamoja na mwanaharakati wa mazingira mkoani Iringa ambaye pia ni
mjumbe wa kamati ya siasa ya mkoa wa Iringa inayomaliza muda wake, Godfrey
Mosha.
Mosha ametupa karata yake hiyo kwa mara
ya pili baada ya kuangushwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Jesca
Msambatavangu katika uchaguzi wa mwaka 2012 kwa tofauti ya kura 17.
Wengine ni pamoja aliyekuwa Katibu wa
Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, George Mlawa, Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Kilolo anayemaliza muda wake, Seth Motto na Evans Balama aliyewahi
kuwa mkuu wa wilaya mbalimbali ikiwemo ya Mbeya.
Wengine ni Ephraim Mhekwa, Listen Mpesa,
Yusitino Mdesa, Daniel Kidava, Albert Chalamila, Joseph Luwahgo, Yohanes Kaguo,
Ramadhani Msigwa na Kelvin Robert.
Kwa upande nafasi moja ya mjumbe wa
halmashauri ya kuu ya Taifa aliyejitokeza ni Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM
Mkoa wa Iringa Salim Abri, Mjumbe NEC Mufindi na mjumbe wa NEC Iringa Manispaa,
Mahamudu Madenge.
Wengine ni Adestino Mwilinge, Asadi
Kikunile, Mgabe Kihongosi, Thom Masini, Enock Ugulumu, Evans Balama, Godfrey
Mgongolwa, Obeid Malima na Michael Mlowe.
Kwa upande wa Katibu wa Itikidi Siasa na
Uenezi, Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa aliwataja waliojitokeza kuwa ni pamoja na
Asad Kikunile, Mwinyikheri Baraza, Michael Mlowe, Denis Lupala, Ibrwahim
Ngwada, Joseph Mgongolwa, Ally Msigwa, Josia Kifunge, Thadeus Tenga, Pius
Njechele, Thobias Kikula, Andre Gemela, John Kiteve, Nasho Kayoka na Godfrey
Mosha.
Magala aliwataka wagombea hao kuwa
watulivu wakati wakisubiri vikao vya juu kuchuja majina yao na kuzingatia
kanuni zinazowazuia kwa namna yoyote ile kufanya kampeni kabla ya mchujo huo.
Wakizungumzia wagombea hao pamoja na wale
waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali katika ngazi ya wilaya, baadhi ya
wanachama wa CCM waliomba vikao vinavyohusika kuwa makini katika kufanya mchujo
ili wapatikane wagombea wanye nia njema na chama hicho.
“Kuna baadhi ya wagombea kwa mfano katika
Manispaa yyetu ya Iringa kuna wagombea ambao wana damu ya upinzani, wakipita na
wakachaguliwa inaweza kuhatarisha shughuli za chama,” alisema mmoja wa wana CCM
aliyejitambulisha kwa jina la George wa kata ya Makorongoni.
Alisema zipo taarifa zisizo rasmi
zinazozungumzwa katika maeneo yasio rasmi kwamba baadhi ya wagombea
waliojitokeza wameshawishiwa na vyama vya upinzani kama mkakati wao wa
kuendelea kuihujumu CCM mjini Iringa na mkoani kwa ujumla.
Naye Peter Makongwa wa kata ya Kihesa alisema CCM mkoani Iringa inahitaji viongozi wenye uwezo na nafasi ili kukabiliana na nnguvu ya upinzani hasa katika jimbo la Iringa mjini ambalo CCM waliangushwa vibaya katika chaguzi mbili zilizopita za udiwani na ubunge.
0 comments:
Post a Comment