METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, May 22, 2017

SHAKA AZIPAISHA JUMUIYA ZA VIJANA ANGOLA

Na Mwandishi Wetu, Luanda

Jumuiya ya Umoja  wa Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) imefanya mazungumzo muhimu na jumuiya za vijana kwa vilivyokuwa vyama vya Ukombozi Kusini  mwa Afrika mjini hapa.

Jumuiya hizo ni pamoja na  vijana wa Swapo ya Namibia  , ANC Youth League ya  Afrika Kusini, Ojm ya Msumbiji, JMPLA ya Angola na ZANUPF youth League ya Zimbabwe.

Akizumgumza kwa bila kugusia agenda za  mkutano wa Luanda  alisema mazungumzo yao nje ya ajenda za kikao kilichowakutanisha vijana mjini Luanda, Angola, alisema jumuiya hizo sasa zitafungua milango ya uratibu na ushirikino  zaidi .

Aliitaja milango hiyo ni ya kudumisha mahusiano na ushirikiano , uimarishaji mikakati na kujenga uwezo kwa vijana kusini mwa Afrikab kulingana na mahitaji ya wakati katika muktadha wa kushamirisha misingi ya uzalendo, demokrasia , nidhamu na ushiriki wa vijana katika kufanya kazi .

"Tumeteta na kutazama hali ya mmomonyoko wa madili uliopo kwa misingi ya uzalendo, kukithiri kwa ufisadi, rushwa,vijana kuandamwa na uvivu wa kutofanya kazi , athari za  dawa ya kulevya na matumizi bora ya rasilimali katika fursa za ajira "Alieleza Shaka.

Alisema masuala hayo ni  pamoja utetezi wa haki za binadamu, maendeleo ya watu , utawala bora na utawala wa sheria ni katika mambo muhimu ya kufanya Afrika ijitanue na vijana wake kujitambua
kifkra, kifalsafa na kiutikadi.

Kaimu huyo Katibu mkuu alisema kwa kadri kizazi cha viongozi walioshiriki ukombozi kusini mwa Afrika na Afrika yote kinavyozidi kutoweka, njia pekee ilio bora na muhimu ni kizazi kipya kujiongeza kimawazo, na kujiandaa kitaaluma .

"Tumejadili kwa kina masuala kuhusu miingiliano ya kibiashara na nafasi za vijana kujijenga kiuchumi, mkakati wa vijana kutoghilibiwa katika masuala
uhalifu, uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya pia hatma ya uongozi na usalama wa watu "Alisema Shaka

Aidha alisema masuala  hayo na mengine kadhaa yatajadiliwa kwa kina katika sekretetieti za jumuiya na mabaraza makuu yake kwa
nchi wanachama na kila jumuiya ili katika vikao vijavyo yaweze kupimwa na kutazamwa kwa kina na vyama  kujulishwa.

"Tumeshaamka na kujiuliza ilikuwaje kina Mwalimu   Nyerere, Dk  Neto, Dk Khama , Jamal Abdi Nasser ,Samoa Machel  mfalme  Haile Sellasie na Ahmed sekou Toure walifanya mambo makubwa na kuacha alama pana Afrka, tumeahidi kufuata nyayo za viongozi wa nchi tano zilizokuwa mstari mbele  katika ukombozi "Alieleza .

Alisema maazimio ya  msingi yaliotokana na ajenda za mama za kikao ambazo zilijadiliwa , ushauri, mbinu na mikakati yake itabaki kuwa siri ya vikao na haitatwekwa bayana kwa wakati huu  hadi watendaji wa  jumuiya watakapokutana katika mkutano ujao  huki Namibia  baadae mwaka huu .Kidumu Chama Chamapinduzi Ccm Na Jumuia zake zote Bara na Visiwani viva Vijana viva.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com