Na Mwandishi Wetu, Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo leo amekutana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Ndg. Thobias Andengenye ofisini kwake.
Katika mazungumzo yao wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika kufanya kazi na pia jeshi la zimamoto na uokoaji wameomba ushirikiano toka kwa mkuu wa mkoa ili kuweza kuliunganisha jeshi hilo na mamlaka za serikali za mitaa ili liweze kufanya shughuli zake kwa ufanisi kwani mnufaika mkubwa wa huduma zao ni mamlaka hizo husika.
Mhe. Mrisho Gambo ametoa rai kwa Jeshi hilo kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala ya kusubiri matukio ya ajali za moto kutokea wanapaswa kutoa elimu kwa wananchi namna ya kuyazuia matukio hayo na kwa kufanya hivyo watapunguza sana kazi yao kwani majanga ya moto yatakua historia.
Pia wamekubaliana kuhakikisha ramani za majengo na michoro ya mpango kabambe (master plan) kwa jiji la Arusha zinapitiwa, lengo ni kuona mapungufu ya kiusalama dhidi ya majanga ya moto na kuona namna ya kuzitatua mapema.
Mkoa wa Arusha hasa kwa jiji la Arusha ni miongoni mwa maeneo ambayo kuna changamoto kubwa sana hasa panapotokea majanga ya moto kwani miundo mbinu na vituo vya zimamoto havitoshelezi mahitaji.
0 comments:
Post a Comment