METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, April 8, 2017

DC UBUNGO AWASIHI WATANZANIA KUFANYA MAZOEZI ILI KUEPUKA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA


Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akiongoza mazoezi ya kukimbia umbali wa Kilomita 6 Leo Jumamosi April 8, 2017 Jijini Dar es salaam
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kufanya mazoezi ya viungo Leo Jumamosi April 8, 2017 Jijini Dar es salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori Wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kufanya mazoezi ya viungo Leo Jumamosi April 8, 2017 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ubungo Plaza
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kufanya mazoezi ya viungo Leo Jumamosi April 8, 2017 Jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akishiriki kwenye mazoezi ya viungo Leo Jumamosi April 8, 2017 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ubungo Plaza
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kufanya mazoezi ya viungo Leo Jumamosi April 8, 2017 Jijini Dar es salaam
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kufanya mazoezi ya viungo Leo Jumamosi April 8, 2017 Jijini Dar es salaam
Afisa Utumishi Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Ndg Ally Ally akishiriki kwenye mazoezi ya viungo Leo Jumamosi April 8, 2017 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ubungo Plaza
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akiwa kwenye mazoezi ya kukimbia Leo Jumamosi April 8, 2017 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ubungo Plaza, Kulia kulia kwake ni Elizabeth Masaba Mkurugenzi wa Kampuni ya POWER ON FITNESS GYM, Mwigine ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg Ndg James Mkumbo
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori Wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kufanya mazoezi ya vioungo Leo Jumamosi April 8, 2017 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ubungo Plaza, Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo, Mwingine ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg Ndg James Mkumbo
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kufanya mazoezi ya viungo Leo Jumamosi April 8, 2017 Jijini Dar es salaam
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kufanya mazoezi ya viungo Leo Jumamosi April 8, 2017 Jijini Dar es salaam
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kufanya mazoezi ya viungo Leo Jumamosi April 8, 2017 Jijini Dar es salaam
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kufanya mazoezi ya viungo Leo Jumamosi April 8, 2017 Jijini Dar es salaam

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Watanzania wametakiwa kujitokeza kufanya mazoezi walau Mara mbili kwa wiki ili kuepuka na kukabiliana na ukubwa na tatizo la magonjwa ya kuambukiza yanayoathiri kwa kiasi kikubwa Duniani.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori Wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kufanya mazoezi ya vioungo Leo Jumamosi April 8, 2017 yaliyoandaliwa na Kampuni ya POWER ON FITNESS GYM kwa kushirikiana na Wilaya ya Ubungo ambapo yalianza kwa Mazoezi ya kukimbia umbali wa Kilomita sita kwa kuanzia katika Viwanja vya shule ya Msingi Ubungo Plaza kupitia barabara ya Sinza-Mwasiliano na hatimaye Barabara ya Ubungo-Shekilango na kurejea katika Viwanja hivyo.

Mhe Makori amesema kuwa magonjwa yasiyoambukiza ni tatizo linalokuwa kwa kasi Duniani ikiwemo nchi ya Tanzania ambapo ameongeza kuwa Magonjwa hayo yamekuwa yakiongezeka kila siku.
Alisema kuwa Tanzania imeridhia kutekeleza mkakati wa miaka minne wa kimataifa uliopendekezwa na shirika La afya duniani (WHO) wa kuzuia mago njwa hayo.

Ameyataja magonjwa hayo yasiyoambukiza yanayowakabili wananchi Duniani kote yatokanayo na kutofanya mazoezi kuwa ni pamoja na Kisukari, Shinikizo La damu, Magonjwa ya Moyo, Saratani, Magonjwa ya akili pamoja na Magonjwa ya Kinywa.

Dc Makori alisema kuwa Kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa na Shirika La afya Duniani (WHO) zimeeleza kuwa Asilimia 63 ya vifo vyote Duniani vilisababishwa na Magonjwa yasiyoambukizwa, asilimia 80 ya vifo hivyo mwaka 2008 vilitokea katika nchi zenye uchumi wa chini na kati ambapo nusu ya vifo hivyo katika nchi zenye uchumi wa chini na kati vikitokea kwa watu wenye umri chini ya miaka 70.

Kwa mujibu wa Takwimu za shirika la afya Duniani kwa upande wa Tanzania inakadiriwa kuwa asilimia 27 ya vifo vyote vilivyotokea vilichangiwa na Magonjwa yasiyoambukizwa mnamo mwaka 2010 huku vifo 76 kati ya watu 1000 ambao ni wanaume na vifo 29 kati ya watu 1000 ambao ni wanawake vilitokea Kwa watu wenye umri chini ya miaka 60 mwaka 2008.
 
Dc Makori amebainisha kuwa bila kuwa na mpango madhubuti wa kupunguza vifo hivyo vitokanavyo na magonjwa yasiyoambukiza huenda tatizo la magonjwa kama Kisukari litaongezeka kutoka watu milioni 366 wanaoishi na ugonjwa huo mwaka 2011 kufikia watu milioni 522 ifikapo 2030.

Aidha Kwa upande wa wagonjwa wenye shinikizo la damu mwaka 2000 watu milioni 900 idadi hiyo itaongezeka mpaka watu bilioni 1.56 ifikapo 2025.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa Kwa kila mwananchi kufanya mazoezi ili kuzuia magonjwa yasiyoambukiza hususani ugonjwa wa Kisukari na Shinikizo la damu.

MD Kayombo amesema kuwa kufanya mazoezi kutaimarisha umoja na mshikamo sambamba na kuimarisha afya za wananchi jambo ambalo litapelekea Taifa letu kuwa na watu wakakamavu ambao wataweza kuisaidia serikali kufikia kusudio lake la kuwa na Tanzania ya viwanda.

Maadhimisho ya Mazoezi ya viungo kwa utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan la kufanya mazoezi kila Jumamosi ya pili ya Mwezi yamefanyika Jiji Dar es salaam ambapo kimkoa yamefanyika Katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ubungo Plaza.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com