METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, March 31, 2017

KAMATI YA BODI YA VILEO YAPITISHA MAOMBI YA LESENI ZA VILEO

Leo hii 31/3/2017 kamati ya bodi ya vileo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imepitisha maombi ya leseni za vileo 520.

Katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo wajumbe kwa pamoja walipitia agenda za kikao ikiwemo agenda ya kupitisha maombi hayo.Maombi hayo ni yale ya leseni za msimu wa April mpaka september 2017 ambapo msimu wa leseni hizi huisha kila baada ya miezi sita ,kwa msimu uliopita leseni zimeisha rasmi leo 31/3/2017.

Akizungumza katika kikao hicho katibu wa bodi hiyo Ndg Peter Ngoti amewaeleza wajumbe kuwa maombi hayo yatazidi kuongezeka kwani hizi ndizo tarehe za wafanyabiashara wanamiminika kwa ajili ya kuja kuhuisha leseni zao na idadi ya  maombi  huzidi zaidi mara baada ya kuisha kipindi cha nyongeza cha siku 21 mara baada ya kufika tarehe ya kwisha leseni ambayo ni 31/3/2017,hivyo wanategemea maombi kuendelea kuwa mengi zaidi .Akiongeza katika hili alisema operesheni maalum itafanyika mara baada ya muda wa nyongeza (grace period) kwisha ili kubaini wasio na leseni na wale wanaofanya biashara kwa kificho  kuwachukulia hatua za kisheria na kuwataka walipe mara moja.

Mjumbe Diwani Mh. Liberata alipongeza operation ya ukusanyaji mapato inayoendelea hivi sasa katika manispaa Ubungo kwa watendaji wa Manispaa na wataalam kufanya ukaguzi duka kwa duka na katika biashara mbalimbali kukagua wasio na leseni na kuhakikisha wanalipia ,na wakati huo huo alitaka kujua kuna mkakati gani juu ya grocery zinazofanya biashara usiku kwa kujificha kuhakikisha wanakata leseni.Akijibu na kufafanua kuhusu hilo Afisa Biashara Ndg Ngoti alisema tayari mkakati upo umeandaliwa kwa kushirikiana na   wenyeviti kubaini watu hao mkakaati huo wana matumaini utaleta tija.

Wajumbe walimalizia kwa kusisitiza kufanya ukaguzi zaidi kubaini idadi zaidi ya mabaa hasa maeneo ya Sinza ,saranga na kimara ambapo imebainika kuna baa nyingi sana ukilinganisha na idadi iliyobainika sasa.

Huu ni msimu unaoanza kwa upande wa leseni za vileo ambapo kila mfanyabiashara wa vileo anatakiwa kugakikisha anahuisha leseni yake mara moja ili kuepuka adhabu za faini au kufungiwa biashara,hivyo wafanyabiashara wote wanatakiwa kuwahi kulipia leseni zao.

LIPA KODI KWA MAENDELEO YA HALMASHAURI YAKO.
Ubungo ya tofauti

IMETOLEWA NA KITENGO CHA UHUSIANO UMC

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com