Na Jumia Travel Tanzania
JUMAPILI
hii ya Desemba 25 ni sikukuu ya Krisimasi ambapo wakristo nchini
wataungana na wenzao duniani katika kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa
bwana wao Yesu Kristo.
Kwa
kawaida sikukuu hii husherehekewa kwa watu kujumuika na familia zao
ambapo hukusanyika kwa pamoja nyumbani, kusafiri, kufurahia chakula,
vinywaji, kupeana zawadi pamoja na burudani nyinginezo walizoziandaa.
Jumia
Travel (www.travel.jumia.com) ingependa kukupendekezea namna mbalimbali
nyingine tofauti na ulizozizoea za kufurahia sikukuu hii mashuhuri
duniani na kuifanya iwe ya kuikumbuka zaidi katika maisha yako.
Ipeleke familia yako kwenye Seafood Gala
Siku ya
Krisimasi bendi ya Skylight itakuwa pale kwenye ufukwe wa Escape One
uliopo Mikocheni kusherehekea sikukuu ya Krisimasi. Litakuwa ni tukio
zuri kwani litajumuisha shughuli tofauti zitakazolenga kila rika kama
vile vyakula vya baharini, michezo ya watoto, muziki wa bendi na kutoka
kwa ma-DJ maarufu jijini Dar es Salaam.
Washuhudie
kwa mara ya kwanza WCB kwenye jukwaa moja Pengine hili ni tamasha kubwa
la kufungia mwaka ambalo lililokuwa likisubiriwa na mashabiki wengi wa
muziki nchini. Mwanamuziki maarufu na mwenye mafanikio zaidi nchini
Tanzania na Afrika ya Mashariki kwa ujumla anatarajiwa kudondosha
burudani ya aina yake akiwa na wasanii waliomo kwenye lebo yake ya
muziki ya WCB ambao ni Harmonize, Rayvanny, Rich Mavoko na Queen
Darleen. Tamasha hilo limepewa jina la ‘Wasafi Beach Party’ na
linatarajiwa kufanyika siku ya Desemba 24, 2016 katika hoteli ya nyota
tatu ya Jangwani Sea Breeze Resort ambapo tayari kuna orodha ya wasanii
na watu maarufu kadhaa tayari wamethibitisha kuwepo.
Nenda
kafurahie bufee la maana kwenye mgahawa unaozunguka wa Akemi Jaribu
kuinogesha Krisimasi hii kwa kwenda kufurahia chakula kwenye mazingira
tofauti na nyumbani. Akemi ni mgahawa pekee unaozunguka nchini Tanzania
ukiwa unapatikana kati ya majengo marefu jijini Dar es Salaam, Golden
Jubilee Tower, ikikupatia fursa ya kujionea jiji hilo ukiwa ghorofani
huku ukifurahia vyakula, vinywaji, muziki na mazingira tulivu na ya
kifahari ukiwa pale.
Double
Tree Hotel watakuwa na Festive Fun Hoteli ya Double Tree by Hilton ya
jijini Dar es Salaam ambayo unaweza kuipata kupitia mtandao wa Jumia
Travel (www.travel.jumia.com), inapatikana katika mazingira tulivu
pembezoni mwa kitongoji cha Msasani ambapo utaweza kufurahia mandhari
nzuri ya bahari pamoja na bustani nzuri. Kipindi hiki cha msimu wa
Sikukuu za Krisimasi, Boxing Day mpaka Mwaka Mpya wameandaa ‘Festive
Fun’ yenye ofa kadha wa kadha za vyakula, vinywaji na muziki mzuri wa
disco la nguvu la kukuburudisha.
Tembelea
majumba ya sinema Wewe kama ni mpenzi wa filamu basi sikukuu hii itaenda
vizuri kwako kwani kutakuwa na filamu mpya na kali ambazo zinatoka
kipindi hiki. Filamu hizo ni kama vile Assassin’s Creed, Passengers na
Why Him? Majumba ya filamu kwa hapa nchini ya Century Cinemax
yanapatikana katika mikoa ya Dar es Salaam (Mlimani City, Dar Free
Market Oyster Bay na Mkuki House Mall) na Arusha hivyo unaweza
kuyatembelea ili kuzifaidi katika kipindi hiki.
0 comments:
Post a Comment