Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa ameongea na Mabalozi na Wawakilishi wa
wafanyabishara Ikulu jijini Dar es Salaam kutoa taarifa ya tatemeko la
ardhi na maafa yaliyotokana tarehe 10 September 2016.
Waziri
Majaliwa amewaomba wawakilishi hao kutoa misaada mbalimbali ili
kuungana na Serikali kuwasaidia walioathirika mkoani Kagera.
Baadhi ya Taasisi na Balozi zilizo ahidi kutoa michango ni:-
Ubalozi wa China – Milioni 100
Ubalozi wa Kuwait – Euro 10,000
Ubalozi wa Kenya- wametoa mabati na malazi
Kampuni ya China Mercharnt Group – Mil 100
Mo Dewji – Milioni 100
Toyota Ltd – Milioni 10
TBL – Milioni 100
Woolworth -Milioni 20
Sahara Tanzania – Milioni 20
Azania Group – Milioni 20
Kagera Sugar -Milioni 100 na Tani 10 za sukari
Nosime Group- Milioni 75
Tanga Cement – Mifuko 1000 ya Saruji
Reginald Mengi – Milioni 110
Protas Ishengoma- Wakili na mhanga wa tetemeko Milioni 5
GBP, MOIL,&OILCOM- Watajenga shule mbili zilizoharibika
Vile
vile Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ametangaza matembezi ya
kukumbuka janga hilo na kuahidi wananchi wote na mashirika mbalimbali
kujitokeza katika matembezi hayo yatakayo fanyika siku ya Jumamosi
asubuhi katika maeneo ya Masaki.
Taarifa zaidi za Matembezi haya zitatolewa katika vyombo vya habari.
0 comments:
Post a Comment