METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, September 23, 2016

LIPULI YASUBIRI POINTI TATU ZA AFRICAN SPORTS KWA SHAUKU KUBWA



NA RAYMOND MINJA IRINGA 

Timu ya Lipuli FC(Wanapuliengo )yenye maskani yake mjini Iringa imepania kuzinyakuwa pointi tatu kutoka kwa African  Sports, ambao watakutana katika mchezo wa kwanza wa Ligi Daraja la kwanza Tanzania Bara ,unaotarajiwa kuchezwa September 24 mwaka huu katika uwanja wa kichangani mkoni Iringa .
Akizungumza na Bigwa katibu mkuu wa timu hiyo Wille Chikweo alisema maandalizi yote yameshakamilika ikiwa ni pamoja na kuipokea timu hiyo  kwa heshima ilipotokea jijini Dar Eesalam ilimokuwa imeweka kambi yake kwa muda  na usajili

Chikweo alisema kuwa jambo kubwa wanalojivunia na linalowaminisha kufanya vema na hatimaye kucheza ligi kuu ni kuwa na vijana chipukizi watakaokiongoza kikosi hicho na vijana hao wanacheza kwa nia moja ya kushinda kwa kuwa wameufuta mpira na sio mpira kuwafuata jambo ambalo
linawaminisha  kuwabamiza African Sports katika mchezo wa  kwanza

“Kwanza niwashukuru wadau wote walioshiriki katika kuisaidia lipuli mpaka hapa ilipofika ,nimshukuru Madam Jeska Rais wa lipuli, mwenyekiti Kuyava ,wadau wakubwa wa Lipuli waliotoa hata wazo la kuisaidia lipuli kwani kwa sasa tumeanzisha kampeni ya (SAIDIA LIPULI BUKU) ambapo unaweza kuichangia kwa kupitia simu ya mkonini ambayo ni 0769442945na utakuwa umeisaidialupuli moja kwa moja  kwa kweli wamefanya kazi kubwa sana niwaombe wana Iringa wote kwa pamoja na wanahabiri  tuisadie lipuli iweze kufanya vema na hatimaye tucheze ligi kuu ”

Kwa upande wake Raisi wa heshima wa timu hiyo Jeska Msambatavangu alisema kuwa endapo wanairinga na wadau wa soka wataunganisha nguvu kwa pamoja wanamini timu hiyo itafanya vema na hatimaye kucheza ligi kuu



Jeska alisema kuwa yeye kama mdau wa soka na Rais wa Timu kwa kushirikiana na wadau wote atahakikisha wachezaji wa timu hiyo wakwaziki kwa namna yoyote wakiwa kambi ili isiwe  sababu ya kutokufanya vema wawapo uwanjani


“African Sports kitu gani nyie chezeni soka linaloelewaka hawa tutawaweka pembeni tu tenaq munabahati mumupata mlezi ambaye ni mama unajua mama huwa na huruma kwa wanewe sasa wewe ukoina unahitaji kiatu halafu labda hujapahatika kuniona siku mbili tatu mana niko bize kidogo wewe chora mguu kwenye karatasi waambie hawa viongo mpelekeni mama ahh dakika moja utapata chezeni kabumbu safi ondoeni shaka ”

 Timu hiyo ya Lipuli kwa sasa imrweka kambi yake wilayani kilolo katika kijiji cha kilole ambako huko wamepata udhamini wa nyumba waliyopewa na paroko wa eneo hilo pamoja na uwanja wakisubiri kuja kukipiga na African Sports
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com