Jumla ya wahamiaji haramu 15 kutoka
Ethiopia (walioketi) wakiwa nje ya ofisi ya uhamiaji mkoa mjini
Singida,jana.Vijana hao walikuwa njiani wakielekea Afrika kusini kusaka
maisha. (Picha na Nathaniel Limu)
Idara ya
uhamiaji mkoa wa Singida, imefanikiwa kukamata vijana wahamiaji haramu
15 kutoka nchini Ethiopia, kwa tuhuma ya kuingia na kuishi nchini bila
kuwa na vibali halali.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake juzi,Afisa Uhamiaji mkoa wa
Singida,DCIS Faith Ihano,alisema wahamiaji hao haramu,wamekamatwa
Februari, 12 mwaka huu saa 12.00 jioni Unyankindi mjini hapa.
Alisema
wahamiaji hao wamekamatwa wakiwa wamefichwa kwenye nyumba ya mtu binafsi
Unyankindi mkabala na kota za nyumba za shirika la nyumba taifa (NHC).
“Kwa sasa
tunamshikilia mwenye nyumba huyo kwa mahojiano zaidi na pindi
upelelezi/uchunguzi utakapokamilika,tutamfikisha mahakamani kujibu
tuhuma inayomkabili ya kupokea na kuhifadhi wahamiaji haramu,” alisema
Ihano.
Aidha
Afisa huyo alisema katika kipindi kifupi cha kati ya disemba na januari
mwaka huu,wamefanikiwa kukamata wahamiaji haramu 30 kutoka Congo, Malawi
na Ethiopia.
“Hii
biashara haramu ya kusaidia na kuhifadhi raia wa kigeni wanaoingia
nchini kinyume na taratibu na sheria,inafanywa na Watanzania wachache,”
alifafanua.
Ihano
alitumia fursa hiyo kuwaasa Watanzania wachache wanaojihusisha na
biashara hiyo haramu,kuacha mara moja,vinginevyo
wakibainika,watachukuliwa hatua kali za kisheria.
0 comments:
Post a Comment