Sunday, March 12, 2023

KAMATI YA BUNGE YA TAMISEM IKIONGOZWA NA DENNIS LONDO YAPOKEA TAARIFA YA MUUNDO NA MGAWANYO WA MAJUKUMU YA OR- TAMISEMI

 










Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Dennis Londo, Mbunge wa Mikumi imepokea na kujadili Muundo na mgawanyo wa majukumu ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 11 Machi 2023 Bungeni jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi, Menejimenti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe, Angellah Kairuki.

Pamoja hayo, Kamati imepokea taarifa ya Utekelezaji wa Miradi tisa ya maendeleo itakayotembelewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI kuanzia tarehe 14 -19 Machi 2023.

Kamati za Kudumu za Bunge zinaendelea na vikao ambavyo vimeanza tarehe 10 Machi 2023 na vinatarajiwa kumalizika tarehe 31 Machi 2023 kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Bunge.

No comments:

Post a Comment