Monday, March 13, 2023

HALMASHAURI ZA SINGIDA KULIPISHWA FEDHA IWAPO ZITASHINDWA KUGAWA MBEGU ZA ALIZETI ZA RUZUKU KWA WAKULIMA

 

Wenyeviti wa Halmashauri za Mkoa wa Singida wakiwa kwenye kikao cha Ushauri cha Mkoa RCC kikao hicho kimefanyika Jumamosi Machi 11, 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Mkoa wa Singida.

Mkuu wa Mkoa wa Peter Serukamba akizungumzia suala la ugawaji mbegu za ruzuku za alizeti kwenye kikao cha RCC juzi Machi 11, 2023.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda akichangia hoja juu ya ugawaji wa Mbegu za Ruzuku za Alizeti kwa wakulima.kwenye kikao cha RCC mkoa wa Singida.

Wajumbe wa Kikao cha Ushauri cha Mkoa RCC wakifuatilia taarifa mbalimbali kwenye Mawalisho.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Innocent Msengi akichangia Hoja kwenye Kikao cha RCC Mkoa wa Singida.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Elia Digha akichangia Hoja kwenye Kikao cha RCC Mkoa wa Singida.


Katibu Tawala anayesimamia Maendeleo ya Kilimo na Uchumi Mkoa wa Singida Stanslaus Choaji akisoma ripoti kuhusu utekelezaji wa shughuli za Kilimo ikiwemo mazao ya Kimkakati.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida Jeshi Lupembe akichangia hoja kwenye Kikao cha RCC Mkoa wa Singida.



Na Hamis Hussein - Singida

MKUU wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba ameziagiza Halmashauri zote mkoani humo kuongeza kasi ya kugawa mbegu za rukuzu za alizeti kwa wakulima kabla ya msimu haujamalizika ili kutimiza lengo la Mkoa la kulima Ekari laki 631391 mwaka huu vinginevyo zitatakiwa kuzilipia Mbegu hizo kwa wakala wa Mbegu za Kilimo ASA.

RC Serukamba ametoa agizo hilo Jumamosi Machi 11, 2023 kwa halmashauri baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya kilimo ya Mkoa kwenye kikao cha ushauri RCC, ambapo ripoti hiyo imeonyesha kuwa bado tani 101.799 kati ya tani 395.38 hazijawafikia wakulima hivyo mkuu huyo akatumia wasaa huo kumwagiza Katibu Tawala anayesimamia eneo la Kilimo na Uchumi Stanslausi Choaji kufuatilia ugawaji wa mbegu hizo.

Serukamba alisema kuwa Halmashauri zitakazoshindwa kuzigawa mbegu zilizosalia kwa wakulima zitatakiwa kuwalipa fedha wakala wa mbegu za kilimo ASA kufidia mbegu ambazo hazitachukuliwa na wakulima.

“Unajua Wizara ya kilimo imetupendelea sisi juzi amenipigia Waziri ananiambia ‘Peter hivi kweli nasikia kuna watu hawajagawa mbegu?’ na nikiwaangalia sababu zenu wala hakuna anayesikitika simply because hulimi wewe sasa zile halmashauri ambazo haziwezi kugawa na mnaona kuna halmashauri inaweza kugawa zipelekeni huko lakini wale ambao hawawezi kuzisambaza Walipe fedha za ASA” alisema RC Serukamba.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida alionyeshwa kutofurahishwa kwenye kikao hicho kilichofanya Jumamosi ya Machi 11 na amemwagiza Katibu Tawala anayesimamia Maendeleo ya Kilimo na Uchumi  kuzifuatilia Halmashauri hizo kujiridhisha na zoezi hilo la  Ugawaji wa mbegu na kusema kuwa endapo halmashauri itashindwa kugawa mbegu hizo kwa muda uliobakia zitanyang’anywa hatimaye zitalazimika kulipa fedha kwa Wakala wa Mbegu za Kilimo.

Aliongeza kwa kuwasisitiza viongozi wa Mkoa wa Singida kutoka maofisini na kwenda kuwasikiliza na kutatua kero za wananchi badala ya kuwa na ubinafsi ambao unarudisha nyumba maendeleo kwa wananchi.

“Tutaonekana watu wa ajabu tusiosaidia watu, hii Level ya ubinafsi imezidi haiwezekani, tusikaeni maofisi jamani hapa ni kwamba nyie mkishawapelekea watendaji wa vijiji kazi yako imeisha mtendaji amefanya you don’t care, ndio style yetu na inawezekana kuna Wakurugenzi, Wenyeviti wa halmashauri hapa kwenye hii ripoti  walikuwa hawajui kama mbegu hazijagawanywa”Aliongeza RC Serukamba.  

Awali Akisoma Ripoti hiyo ya Kilimo mwishoni mwa Juma lililopita Katibu Tawala wa Maendeleo ya Kilimo na Uchumi Stanslaus Choaji amesema hadi kufikia mwezi Februari Mwaka huu Mkoa ulikuwa umetekeleza asilimi 75.9% kwa kulima Ekari  479855.75 za zao la alizeti ambapo Mkoa umepokea mbegu za ruzuku za alizeti aina ya Record tani 395.38 na tayari tani 293.581 zimewafikia wakulima.

Choaji alisema katika ekari zilizolimwa hadi sasa endapo hali ya hewa ikiendelea vizuri mkoa utaweza kuvuna tani 317297.2 sawa na asilimia 64.4 % kati ya lengo la kupata tani 492486 kwa Msimu huu wa kilimo.

Suleiman Mwenda Mkuu wa Wilaya ya Iramba akizungumza kwenye kikao hicho akachangia juu ya ugawaji wa mbegu hizo ambapo amesema hivi karibu alifanya mkutano na wananchi wa Mgongo na Shelui ambapo Mkulima alilalamika kukosa mbegu hizo za ruzuku akidai kuwa wakulima wamekuwa wakitakiwa kulipia fedha Taslimu badala ya kukopeshwa kama ilivyoelekeza serikali.

Baadhi ya Wenyeviti wa halmashauri wametaja changamoto zilizopelekea kushindwa kugawa mbegu zilizo salia kwa wakulima sababu hizo ikiwa pamoja na  hali ya hewa kubadilika  ambapo mvua kukatika jambo lililopelekea wakulima kushindwa kulima.

No comments:

Post a Comment