Monday, November 29, 2021

MAJALIWA AKAGUA UJENZI WA BARABARA YA CHUNYA – MAKONGOROSI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na fundi mkuu wa ujenzi wa madarasa katika Shule ya Sekondari ya  Kipoka wilayani Chunya, Stephen Mpagazi  (kulia) wakati alipokagua ujenzi huo akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya Novemba 29, 2021.  Wengine kutoka kushoto ni  Mbunge wa Lupa, Masache Kasaka, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mbeya  Mchungaji Jacob Mwakasole na wa pili kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kipoka Simon Shimwela. 

Muonekano wa kipande cha barabara ya Chunya – Makongorosi yenye urefu wa Kilomita 39 ambao unatarajiwa kukamilika  Februari 2022 ambayo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua maendeleo ya ujenzi wake, 

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Mji Mdogo wa Makongorosi wilayani Chunya Novemba 29, 2021 wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa  barabara ya Chunya – Makongorosi yenye urefu wa Kilomita 39 ambao unatarajiwa kukamilika  Februari  2022 . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment