Saturday, February 29, 2020

UKEREWE YAZINDUA ZOEZI LA UPULIZAJI WA KIUATILIFU CHA KUUA MBU MAJUMBANI


Jumla ya Nyumba 87,599 zilizopo kwenye Kata 25, wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza zinatarajiwa kupuliziwa kiuatilifu cha Kuua Mbu majumbani kwa lengo la kupambana na maambukizi ya Maralia .

Unyunyuziaji huo unaotekelezwa Na Serikali kwa kushirikiana Na shirika la Abt associates chini ya ufadhili wa serikali ya Marekani kupitia USAID ni Mpango wenye gharama kubwa Na matokeo ya haraka katika kudhibiti Ugonjwa wa maralia,  zoezi linalotajaiwa kuanzia tarehe 3 March,  2020.

Akizungumza na waandishi wa habari February 28, 2020 wakati wa  uzinduzi wa zoezi hilo uliofanyika Wilayani humo  Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Cornel L.B Magembe amewataka wananchi wa Ukerewe katika kata zote ambazo zoezi Hilo litafanyika kutoa ushirikiano kwa maafisa wanaosimamia zoezi Hilo.

Alisema Mkoa wa Mwanza wameendelea kupambana maambukizi ya ugonjwa wa maralia kutoka asilimia 41% ya mwaka 2015/2016 hadi asilimia 15.4% kwa mwaka 2017/2018.

Alizungumzia hatua mbalimbali zilizochukuliwa serikali zikiwemo huduma kwa wagonjwa kwa kutoa dawa za mseto,  ugawaji wa vyandarua bila malipo pamoja na unyunyuziaji wa dawa ya kuja mbu majumbani. 

Akizungumzia zoezi hil,  Mkuu huyo aliwataka watumishi kuhakikisha wanasimamia zoezi Hilo kwa weledi huku akitoa onyo kwa mtumishi yoyote kutohujumu zoezi Hilo ikiwemo kuuza Madawa yanatotumika katika shughuli hiyo.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt Thomas Rutachunzibwa alisema kuwa kwa utafiti walioufanya 2017 wastani wa 51.2% ya wanafunzi wa shule ya msingi Wilaya ya Ukerewe walikutwa na maambukizi, Ndo maana wameamua kuanza na Wilaya ya Ukerewe.

Kwa upande wao mmoja wa watumishi wa zoezi Hilo Juliana Bernard alisema kuwa wao wamejipanga kuhakikisha wanatekeleza majukumu Yao Na kusimamia viapo vyao wakati wote wa utekelezaji wa zoezi hilo. 

No comments:

Post a Comment