Friday, February 28, 2020

DC NJOMBE AAGIZA KUKAMATWA WALIMU WAFANYAYO VITENDO VYA KIKATILI

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Njombe ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Ruth Msafiri akizungumza na wananchi wa Makambako alipokuwa akiupokea msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili.
 
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Njombe ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Ruth Msafiri (kushoto) akisalimiana na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Imelda Kamugisha(kulia)alipokuwa akipokea msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Imelda Kamugisha akielezea lengo la msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wakati msafar huo ulipowasili mkoani Njombe.

Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth Msafiri ameagiza kukamatwa kwa walimu mkoani Njombe watakaobainika kuwafanyia vitendo vya kikatiki wanafunzi ili kukomesha vitendo hivyo vinavyoendelea kutoka nchini.

Hayo yamebainika leo Makambako mkoani Njombe wakati msafara wa kijinsia kutokomeza ukatili ulipofika mkoani humo kwa ajili ya kutoa elimu ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Mhe. Ruth amesema kuwa Serikali haipingi adhabu ya viboko ila sio kutoa adhabu ya  viboko vya kupitiliza na kusababisha vilema na maumivu kwa wanafunzi.

Ameongeza kuwa suala la ukatili ni mapambano makubwa nchini hivyo jitihada zinahitajika kwa wananchi wadau na mashirika yasiyo ya kiserikali kuhakikisha wanaunganisha nguvu pamoja kuondokana na vitendo vya ukatili.

Mhe. Ruth amevitaka vyombo vya usalama kuacha kufanya ukatili kwa kuchelewesha kesi za vitendo vya ukatili wa kijinsia na kusababisha ukatili wa kihisia kwa wahanga wa vitendo hivyo.

“Vyombo vya usalama mnachelewesha kesi mnaomba rushwa nawaomba vyombo vys usalama msiwe kikwazo cha kutopatikana kwa haki ya wahanga wa vitendo vya ukatili” alisema

Akizungumza kuhusu msaada wa kisheria unaotolewa na Shirika la Legal Serivces Facility Joseph Magazi amesema kuwa wameweka nguvu katika kuisidia jamii katika matatizo ya kisheria kwa kuwawezesha wasaidizi wa kisheria katika mikoa na wilaya kutoa elimu husika.

"Tumejipanga kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha tunaifikia jamii katika kutoa elimu itakayowezesha wenye matatizo mbalimbali ya kisheria kupata msaada na kuyatatua matatizo yao" alisema

No comments:

Post a Comment