Rais Mhe.Dkt. John Pombe
Magufuli,akizungumza Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma wakati wa hafla ya
kupokea gawio na michango kutoka katika Taasisi, Makampuni na Mashirika
ya Umma.
Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe.Dkt.Philip Mpango,akizungumza wakati wa hafla ya kupokea gawio na
michango kutoka katika Taasisi, Makampuni na Mashirika ya Umma
iliyofanyika Chamwino Ikulu jijini Dodoma.
Msajili wa hazina nchini
Bw.Athuman Mbutuka,akifafanua jambo wakati wa hafla ya kupokea gawio na
michango kutoka katika Taasisi, Makampuni na Mashirika ya Umma
iliyofanyika Chamwino Ikulu jijini Dodoma.
Baadhi ya Taasisi,Makampuni na
Mashirika ya Umma yakimkabidhi Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli,gawio na
michango katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo.
Sehemu ya washiriki katika hafla
ya kupokea gawio na michango kutoka katika Taasisi, Makampuni na
Mashirika ya Umma wakisikiliza hotuba ya Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli,
Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo.
Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli,akiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya kupokea gawio na michango kutoka
katika Taasisi, Makampuni na Mashirika ya Umma hafla hiyo imefanyika
Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo.
Picha na Alex Sonna
………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Rais Mhe.Dkt.John Magufuli ametoa
siku 60 kuanzia leo Taasisi na Mashirika ya Umma 187 yaliyoshindwa
kukabidhi gawio na michango yao kuhakikisha wanakabidhi gawio hilo
vinginevyo viongozi wake wajiondoe wenyewe.
Mhe.Magufuli ametoa agizo hilo leo
Ikulu jijini Dodoma, wakati wa hafla ya kupokea gawio na michango
kutoka katika Taasisi, Kampuni na Mashirika ya Umma ambapo amepokea
shilingi Trilioni 1.05 kutoka kwa taasisi na mashirika 79 kati ya 266.
Amesema kuwa Serikali imewekeza
shilingi trilioni 59.6 kwa taasisi na mashirika 266 lakini kutokana na
utendaji mbovu,ufuatiliaji dhaifu na vitendo vya wizi,rushwa na
ubadhirifu kwenye mashirika ambayo serikali ina hisa mapato
yaliyokusanywa kupitia uwekezaji huo yalikuwa madogo.
“Hatuwezi kuendelea kuwa na
Mashirika au Taasisi za namna hii, pamoja na wenyeviti wa Bodi,
tunazungumza kila mara hawataki kuelewa, licha ya Serikali kuweka fedha
kiasi cha shilingi trilioni 59.6 ambazo ni fedha za watanzania kama
mtaji katika Mashirika hayo, Waziri Mpango natoa siku 60 kuanzia leo ili
Mashirika haya 187 yaweze kukabidhi kwako gawio” amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amemuagiza
Waziri wa Fedha awaandikie barua wote ambao hawapo kwenye orodha hii,
baada ya siku 60 ambaye hataleta gawio lolote ajihesabu hayupo, kila
siku wanasema wanapata hasara, kila siku ni hasara tu, nchi za
Scandinavia zinaendesha nchi zao kwa sababu ya gawio, wana watu
waaminifu kama nyinyi mlioleta gawio hapa leo.
Rais Magufuli amewapongeza
waliochangia gawio na kusema kuwa waendelee kufanya hivo kwani nchi
haiwezi kuwa na maendeleo kwa kujenga miradi kama vile reli ya kisasa,
kujenga hospitali na shule au mradi wa Bwawa la Nyerere bila kuwa na
fedha ambazo zinakusanywa kupitia vyanzo vya kodi pamoja na gawio au
michango.
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha
na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesena kuwa anawakumbusha watanzania
kuwa uchumi wa Tanzania utajengwa na watanzania wenyewe na hakuna mtu
atakayekuja kulijenga taifa hili.
Waziri Mpango amesema kuwa
katika Serikali ya Awamu ya Tano ukusanyaji wa mapato umeongezeka kwa
kiasi kikubwa ukilinganisha na miaka iliyopita.
“Mapato yaliyotokana na gawio na
michango ya Kampuni, Taasisi na Mashirika yameongezeka ambapo mwaka
2014/2015 ilikuwa shilingi bilioni 161.04 tu, na mwaka 2017/2018
yalikuwa shilingi bilioni 842.13, na kama hiyo haitoshi mwaka 2018/2019
mapato yamefikia shilingi trilioni 1.05, hili ni ongezeko kubwa sana na
linastahili pongezi kwa Serikali yako Mheshimiwa Rais” Mhe. Mpango.
Awali,Msajili wa Hazina,
Bw.Athumani Mbutuka amesema kuwa Serikali imefanya jitihada mbalimbali
ikiwa ni pamoja na kudhibiti matumizi katika Taasisi, Kampuni na
Mashirika ya Umma, ambapo Juni mwaka 2019 Mashirika ya Umma 15
yalipunguzwa hadi kufikia 8 na kupunguza gharama za uendashaji.
Pia ameongeza kuwa katika mwaka
wa fedha unaoishia Juni 30 mwaka huu, Ofisi ya Msajili wa Hazina
imevirudisha viwanda 31 vilivyokuwa havifanyi kazi, pamoja na kurudisha
Serikali viwanja, mashamba na nyumba 337.
No comments:
Post a Comment