Msimamizi Mkuu wa huduma za
matibabu na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU (CTC) Dkt. Onesmo Ng’ande
akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama kuhusu jengo linaloendelea
kujengwa kwa ajili ya utoaji wa huduma za UKIMWI alipotembelea na kuweka
jiwe la msingi ujenzi huo katika Kituo cha Afya cha Ipogolo Iringa.
Mwenyekiti wa NACOPHA, Leticia Kapela akitoa salamu wakati wa hafla hiyo.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista
Mhagama akimjulia hali Mzee Marko Mveyange aliyelazwa katika Kituo cha
Afya cha Ipogolo kwa ajili ya matibabu.
Mwakilishi wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Dawa za Kulevya Mhe.Omari Badwel (Mb) wa
Bahi akitoa salamu za kamati hiyo wakati wa hafla hiyo.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista
Mhagama akipokea maelezo kutoka kwa Dkt. James Mfuse anayesimamia
Maabara ya Kituo cha afya cha Ipogolo kuhusu ujenzi wa Jengo la Kituo
cha utoaji wa huduma za UKIMWI alipotembelea kuweka jiwe la msingi
Novemba 22, 2019.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista
Mhagama akihutubia wananchi wa Ipogolo walioshiriki wakati wa hafla ya
uwekaji wa jiwe la msingi katika Jengo la Kituo cha utoaji wa huduma za
UKIMWI linaloendelea kujengwa katika kituo cha Afya cha Ipogolo mkoani
Iringa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dkt. Leonard
Maboko akizungumza wananchi wa Ipogolo (hawapo pichani) walioshiriki
wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Jengo la Kituo cha
utoaji wa huduma za UKIMWI linaloendelea kujengwa katika kituo cha Afya
cha Ipogolo mkoani Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya
Iringa Mhe. Richard Kasesela akitoa taarifa hali ya UKIMWI katika mkoa
huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Ally Hapi kwa Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista
Mhagama alipotembea mkoani hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasele akitoa salamu za Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo wakati wa hafla hiyo.
************************************
MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameweka
jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Afya Ipogolo Manispaa ya Iringa
ikiwa ni sehemu ya mradi wa uboreshaji wa vituo 20 vitakavyotoa huduma
za UKIMWI kwa wasafirishaji wa masafa marefu.
Hafla hiyo
iliyofanyika tarehe 22 Novemba, 2019 katika Kata ya Ruaha Kijiji cha
Ipogolo mkaoni Iringa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu
wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, Mwakilishi wa Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Dawa za Kulevya
,Omari Badweli (Mb) wa Bahi, Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt Leonard
Maboko, Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe, Mkurugenzi wa Manispaa
ya Iringa, Hamad Ahamad Njovu na wawakilishi kutoka , Ofisi ya Rais
-TAMISEMI , Wizara Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano , Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ,TANROADS pamoja na
watendaji kutoka Halmashauri.
Kabla ya kuweka
Jiwe la Msingi, Waziri Mhagama alipongeza juhudi za Tume ya Taifa ya
Kudhibiti Ukimwi za uratibu na utekelezaji wa masuala ya mapambano dhidi
ya UKIMWI kwa kuhakikisha ujenzi wa vituo 20 unaanza katika maeneo
yenye vichocheo vya maambukizi ikiwemo barabara zinazotumiwa na
wasafirishaji wa masafa marefu.
“Uboreshaji wa
majengo ya Kituo cha Afya cha Ipogolo kwa niaba ya maboresho kama haya
kwenye vituo 20 vilivyoko kando kando ya barabara kuu ya Dar es Salaam
hadi mipaka ya Kasumulu (Tanzania/Malawi) na Tunduma (Tanzania/Zambia)
ili kutoa huduma za udhibiti wa VVU/UKIMWI kwa ufanisi kwa wasafirishaji
wa masafa marefu pamoja na jamii zinazoishi kwenye maeneo hayo
utasaidia kuendeleza mapambano dhidi ya UKIMWI kwa kuzingatia mchango
utakaotokana na ujenzi wa vituo hivi”.
Waziri alieleza,
ujenzi huo unaotekelezwa kupitia programu ya sattf barabara kuu ya Dar
es salaam hadi mipaka ya Tunduma/Nakonde (Zambia) na
Kasumulu/Songwe(Malawi) kwa kutambua umuhimu wa huduma za afya kwa
wananchi wa Tanzania na kwa kuzingatia misingi ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania (1977) pamoja na marekebisho yake. Uboreshaji na
utoaji wa huduma bora kwa wananchi ni moja ya utekelezaji wa haki za
binadamu katika kupata huduma za afya na haki ya kuishi.
Aidha alieleza
kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha wananchi hususani wanaoishi na
virusi vya Ukimwi (WAVIU) wanapata haki ya matibabu ya VVU na magonjwa
nyemelezi, haki ya kutokubaguliwa na haki za kushirikishwa. WAVIU nao
pia wana wajibu wa kulinda wengine wasipate maambukizi ya VVU.
Kwa kuzingatia
Sheria ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI (Kuzuia na Kudhibiti) Na. 28 ya
mwaka 2008 na Sera ya Taifa ya UKIMWI ya mwaka 2001 zote zinatoa wajibu
kwa kila mtu kulinda na kutetea haki za WAVIU.
Naye Mkuu wa
Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akizungumza kwa niaba ya Mkoa wa mkoa
huo Mhe.Ally Hapi alieleza kuwa, ujenzi wa vituo hivyo utasaidia
kupunguza maambukizi na kuongeza tija katika huduma zitakazotolewa
kupitia vituo hivyo.
“Ujenzi wa kituo
hiki uwe chachu ya kuendelea kutumia huduma za Ukimwi ikiwemo matumizi
sahihi ya dawa za kufubaza virusi ili kuendelea kuwa na afya njema na
kushiriki vyema katika shughuli za kimaendeleo nchini’”alisema Kasesela
Kwa Upande wake
Mwenyekiti wa NACOPHA, Leticia Kapela alieleza kuwa, jamii haina budi
kuendeea kuunga mkono jitihada hizo na kuhakikisha tatizo la unyanyapaa
linatokomezwa kabisa na kuendelea kuishi kwa upendo, usawa na amani.
“Uzinduzi wa leo
umeonesha upendo na kujali masuala ya watu wanaoishi na Virusi vya
UKIMWI hiyo niwaombe viongozi wa dini kuungana na jitihada za mapambano
haya kwa kuzitumia nafasi zenu kukemea masuala ya unyanyapaa kwa watu
wanaosihi na maambukizi.
“Viongozi wa dini
tuendelee kuliangalia hili kwa kukemea masuala ya unyanyapaa kwa
malengo ya kuifikia 909090 na ikumbukwe hakuna sababu ya kufanya hivyo
kwa kuzingatia usemi usemao asohili analile,”alisisitiza Leticia.
No comments:
Post a Comment