Baadhi ya wajumbe wa kikundi cha Rose Tweve kilichopo kata ya Nzihi mkoaniri Iringa wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kikao chao cha kikatiba
NA FREDY MGUNDA
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha
mapinduzi (CCM) Rose Tweve ameendelea kuitunisha mifuko ya wanawake wa UWT mkoa
wa Iringa kwa kukuza mtaji walipewa
awali na mbunge huyo.
Akizungumza na blog hii mwenyekiti wa kikundi cha Rose
Tweve, Aulelia Mbembe alisema mbunge wa viti maalum Rose Tweve aliwapa mtaji wa
shilingi laki tano(500,000/=) kwa kuanzia lakini waliunda kikundi na kukiita
Rose Tweve kwa lengo la kumuuezi mbunge huyo kwa mchango wake kwa wanawake wa
UWT kata ya Nzihi mkoani Iringa.
“Mbunge alitupa mtaji lakini tulijiongeza kwa kukopeshana kwa riba ndogo ambayo
tulijipangia sisi wenyewe kwa
kukopeshana na kukutana kwa mwezi mara moja kwa ajili ya kununua hisa pamoja na
kubadilisha mawazo kwa lengo la kukuza mitaji na kufanya maendeleo yetu binafsi”
alisema Mbembe
Mbembe alisema kuwa mtaji wa kikundi cha Rose Tweve
kimefanikiwa kukuza mtaji kutoka shilingi laki tano 500,000/=) hadi kufikia
kiasi cha shilingi milioni kumi laki moja na nusu (10,150,000/=) kwa kipindi
cha miaka mitatu kutoka mwaka 2017 hadi hii leo hapo ndio utajua kuwa
ukimwezesha mwanamke unakuwa umeikomboa jamii.
‘’Kama kikundi tunategemea kuja kuwa
na miradi yetu mikubwa itakayokuwa inaingiza faida kwetu na taifa kwa
ujumla kupitia kulipa kodi kwa miradi hiyo ,lakini tunategemea kutembelea
na kusaidia vikundi vya watu maalumu kama vile walemavu ,yatima ,wazee
wasiojiweza,na waathirika wa vvu,yote haya
ni mchango na matunda ya Mbunge Rose Tweve ,kwa kweli shukrani nyingi zifike kwake ,na viongozi wengine
wachukue mfano wa mbunge dada Rose Tweve
kwa kusaidia jamii kama Rose Tweve
alivyotusaidia sisi kikundi cha akiba
cha wanawake(UWT) Rose Tweve Nzihi ‘’Alisema Aulilelia Mbembe mwenyekiti wa
kikundi hicho.
“Hebu angalia ndugu mwandishi wa habari jinsi gani
wanawake wa UWT kata ya Nzihi tulivyoweza kutumia vizuri fursa tuliyoipata
kutoka kwa mbunge Rose Tweve kwa kutusaidia kubadilisha maisha yetu kwa kuweza
kujikimu kimaisha tofauti na ilivyokuwa hapo awali hivyo tunamshukuru sana
mbunge Rose Tweve” alisema Mbembe
Mery
Msigara ni moja wa wajumbe wa
kikundi cha akiba cha Rose Tweve alisema
kuwa alikuwa anashinda nyumbani kwa
kumtegemea mume wake kwa kila kitu lakini baada ya kujiunga kwenye kikukidi cha
Rose Tweve amekuwa mjasiriamali anayeweza kufanya biashara ndogondogo na
kupata faida kila kukicha huku familia yake ikipata maendeleo ukilinganisha na
awali,yote haya ni matunda ya mbunge Rose Tweve.
Wajumbe katika kikundi hicho wameonekana kuwa na malengo makubwa katika kufanikiwa
huku wakisema kwa mwanga waliooneshwa na
mbunge Rose Tweve wanaamini watafikia malengo yao ya mbali kimafanikio
kupitia kikundi hicho cha akiba cha Rose Tweve .
Hadi sasa mbunge Rose Tweve amefakiwa kuvifikia na kuvitembea jumla ya vikundi 92 vya mkoani iringa na kuviwezesha kama ilivyo kwa hiki kikundi cha kata ya Nzihi.
No comments:
Post a Comment