Wataalam wa Wizara ya Madini katika kikao na kampuni mbalibali zinayokusudiwa kujenga Vinu vya Kuchenjua, Kuyeyusha na Kusafirisha Madini.
Katika
jitihada za kuhamasisha shughuli za Uongezaji Thamani Madini Nchini, kuanzia
tarehe 6 hadi 7 Februari, 2019, Wizara ya Madini ilikutana na baadhi ya Kampuni
zinazokusudiwa kujenga Vinu vya Kuchenjua, Kuyeyusha na Kusafisha Madini
nchini.
Lengo
la wizara kukutana na kampuni hizo ilikuwa ni kuangalia uwezo wa kifedha, tekinolojia
na Utayari wao. Kampuni hizo ni kutoka Ndani na Nje ya Nchi.
Serikali
inahamasisha shughuli za uongezaji Thamani madini kufanyika nchini ili kuongeza
pato, ajira na uhuishaji wa tekinolojia kwa wazawa.
No comments:
Post a Comment