JAPAN WAWADAI ARDHI MAREKANI
AMINI NYAUNGO
Marekani moja ya nchi yenye ujanja sana
haswa katika swala zima la kijeshi wanambinu nyingi sana haswa
inapotokea vita , Japan pia miongoni mwa nchi zilizo vizuri swala zima
la kijeshi, Marekani walichokifanya kuomba hifadhi ya ardhi kwa ajiri
ya watu wake wakijeshi kufanya mazoezi.
Miaka mingi sasa imepita tangu Marekani
iombe kipande cha ardhi kwa ajiri ya wanajeshi na sasa miaka 20 imepita
tangu wachukue, Japan sasa wanataka ardhi yao, Marekani inataraji
kurejesha kipande cha ardhi cha Okinawa kwa Japan kinachosemekana
kuchukuliwa na nchi hiyo miaka ishirini iliyopita.
Eneo hilo limekua likitumika na jeshi
la polisi la Marekani kwa mazoezi mbalimbali ya kijeshi na baada ya eneo
hilo kurudishwa kwa wenye nalo wanajeshi wote watatakiwa kurudi
Marekani. Wananchi wa eneo hilo wamekua wakilalamika juu ya uhamiaji wa
jeshi la Marekani katika eneo hilo kwa muda mrefu sana hivyo kuwazuia
wakazi hao kufanya kazi za kimaendeleo kuongeza kipato chao.
Kutokana na masharti yaliyowekwa na
Marekani,Japan inatakiwa ijenge sehemu kubwa ya kutua helikopta za
kimarekani chini ya utawala wa Wamarekani wenyewe. Sharti hilo
limepingwa na wengi kupelekea kusababisha kusitishwa kwa shughuli hiyo
hadi pale polisi walipoingilia kati na kupambana na maandamano hayo.
No comments:
Post a Comment