Thursday, December 8, 2016

WAZIRI MAKAMBA: SINGIDA ITANUFAIKA NA MRADI WA UMEME WA UPEPO

MARTHA MAGAWA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January  Makamba amesema kuwa mpango wa serikali ni kuwa na vyanzo vingi vya  uzalishaji umeme ili kuwa na vyanzo vya nchi endelevu na kuunga mkono  juhudi za benki ya Dunia kuzalisha umeme wa upepo katika nchi  zinazoendelea ikiwemo Tanzania.makamba-1

Makamba amesema hayo wakati wa Kongamano la wadau wa Nishati ya umeme  walipokutana kuzungumzia matumizi ya Nishati ya umeme inayozalishwa kwa  njia ya upepo itakayounganishwa kwenye gridi ya taifa na mfumo huo utawasaidia wananchi wa Singida .

“Kwa kuwa umeme huo utazalishwa kwenye maeneo ya vijijini, wananchi  wanatakiwa kupata umeme kwa bei rahisi kulingana na uchumi wao na sio  kuuziwa umeme kwa bei juu, na zaidi Wizara yake inapenda kuweka  wazi kuwa huu mradi una faida kubwa sana kulingana na mfumo wa nchi  ulivyo,”amesema Makamba.shante

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuzalisha umeme wa upepo Afrika Mashariki Six  Telecoms,  Rashid Shamte amesema kuwa mfumo huu wa gridi ndogondogo una faida kubwa sana kwa wananchi kwani asilimia kubwa kulingana na ripoti  ya benki ya dunia wananunua umeme wa bei nafuu kwahiyo serikali  imekubaliana na kampuni yetu na imeweza kukubali kuwa mradi huu una  tija na   utasimamiwa na serikali yenyewe kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa  Singida pamoja na Halmashauri.shantee

Kwa upande wa Wizara ya Nishati na Madini, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo  amewataka wawekezaji hao kuuza umeme kwa bei rahisi kwani mara nyingi  mipango ya serikali imekuwa haiendani na mikakati ya wawekezaji kwahiyo wanategemea kuona kuwa mradi huu uwe nafuu ya wananchi wa vijijini  kupata umeme kwa bei rahisi.

No comments:

Post a Comment