Gavana wa
Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Prof. Benno Ndulu akitoa ufafanuzi kuhusu
hali ya kukua kwa uchumi nchini kukanusha taarifa za kuwepo kwa mdororo
wa uchumi nchini Tanzania.Kulia ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mabenki
Bw. Kenedy Nyoni. Na Lilian Lundo na Abushehe Nondo- MAELEZO.
Aidha, amesema kuwa Tanzania ni kati ya nchi kumi bora za Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi ya haraka.
Prof.
Ndulu ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari juu ya hali ya uchumi nchini.
“Kwa
mujibu wa Takwimu ya Ofisi ya Takwimu ya Taifa, hali ya ukuaji wa wa
Tanzania imeendelea kuwa ya kuridhisha, ambapo katika robo ya kwanza ya
mwaka 2016, ukuaji wa pato la Taifa unakadiriwa kuongezeka kwa asilimia
5.5” Prof. Ndulu.
Prof.
Ndulu amezitaja shughuli zinazochangia kasi ya ukuaji wa uchumi kuwa ni
pamoja na sekta ya, kilimo asilimia 11.7, biashara asilimia 10.6,
uchukuzi asilimia 10.1, fedha asilimia 10.1 na mawasiliano asilimia
10.0.
Kwa
mujibu wa Prof. Ndulu amesema shughuli za kiuchumi zilizokua kwa kasi ya
juu zaidi katika robo ya kwanza ya mwaka 2016 ni sekta ya fedha
asilimia 13.5, mawasiliano asilimia 13.4 na utawala wa umma asilimia
10.2.
Kuhusu
mchango wa Sekta mbalimbali katika kuchangia kuleta fedha za kigeni
nchini amesema kuwa Kilimo cha mazao yote kinachangia asilimia 25 ambazo
ni dola za Kimarekani milioni 850, Utalii ukiongoza kwa dola bilioni
2.5, Viwanda dola bilioni 1.5 na dhahabu dola bilioni 2.5, usafirishaji
kwenda nje bilioni 1.1.
Akizungumzia
deni la Taifa, Prof. Ndulu amesema kuwa kiwango cha deni hilo kwa sasa
ni asilimia 20 ya pato la Taifa ambayo si mbaya ikilinganisha na ukomo
wa asilimia 50 ya Pato la Taifa.
Prof.
Ndulu amebainisha kuwa kulingana na tafsiri ya uchumi kuhusu deni hilo,
Tanzania bado ina nafasi kubwa ya kuendelea kukopa bila kuhatarisha
ustahimilivu wa deni hilo.
Katika
hatua nyingine, Prof. Ndulu ametoa ufafanuzi kuhusu mapato katika
bandari ya Dar es Salaam kuwa yameongezeka licha ya kupungua kwa
uingizwaji wa mizigo kupitia bandari hiyo.
Kuhusu
mfumuko wa bei, Prof. Ndulu amesema bei za bidhaa mbalimbali zimeendelea
kushuka na kufikia asilimia 4.9 kwa mwezi Agosti, ambapo kushuka kwa
kiwango hicho kulichangiwa na bei zisizojumuisha vyakula na nishati.
Prof.
Ndulu pia amesema Serikali inaendelea na umaliziaji na uendelezaji wa
miradi mikubwa ya miundombinu ikiwa ni pamoja na mradi wa reli ya kati
kwa kiwango cha kisasa (standard gauge), ujenzi wa bomba la mafuta la
Uganda na upanuzi wa bandari ya Tanga.
No comments:
Post a Comment