SERIKALI imeanza ujenzi wa daraja la kuunganisha vijiji vya lighwa na Ujaire na barabara ya lighwa Ujaire kwa gharama ya Sh. Milioni 345,ambapo kukamilika kwake kutawaondoa wananchi kwenye adha ya kukatika kwa mawasiliano kipindi cha masika.
Daraja hilo linajengwa na Mkandarasi Mzilabwela Company Limited na kusimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA),ambapo kujengwa kwake kunatokana na serikali kusikia kelele za wananchi na za Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu kuhusu kujengwa kwa daraja hilo.
Akizungumza na mtandao huu Octoba 25,2023,Mbunge Mtaturu amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia fedha ziende kutekeleza miradi hiyo ili wananchi wa Kata ya Lighwa na Ikungi kwa ujumla waondokane na changamoto hiyo.
“Kwa jitihada hizi sasa kero ya mto kati ya Lighwa na Ujaire kuunganisha Dung’unyi hadi Ikungi inaenda kuondolewa,kweli Chama Cha Mapinduzi (CCM),kinaendelea kudhihirisha kuwa ni kimbilio la wananchi,Ilani ya uchaguzi iliyonadiwa inatekelezwa kwa kasi kubwa,”amesema Mtaturu.
Diwani wa Kata ya lighwa Gabriel Mukhandi akimpokea mkandarasi huyo alipofika kuanza kazi,amemshukuru Mbunge kwa jitihada zake za kufuatilia changamoto walizonazo wananchi.
“Hatimaye leo mkandarasi amefika kuanza kazi akiwa na vifaa vyote vya ujenzi,ahsante sana Mh Rais Samia kwa kuridhia kuleta fedha Halmashauri ya Ikungi ahsante mbunge wetu Mtaturu hakika umetatua kero iliyotutesa kwa miaka mingi,umesikia kilio chetu maana kupitia ziara zako ulipewa kero hii na kuahidi kuifikisha bungeni leo tunaona matokeo yake,ahsante sana,”.ameshukuru Mtaturu.
Baadhi ya wananchi wakizungumza na mtandao huu wamefurahi na kuonyesha matumaini makubwa na serikali yao inayoahidi na kutekeleza.
No comments:
Post a Comment