Na Saida Issa, Dodoma
CHAMA Cha wafugaji Tanzania (CCWT)kimesema ili kuendelea kutatua migogoro na changamoto ya wafungaji nchini kinakwenda kuzindua kadi za kielektroniki kwa wafugaji na kuwasajili kutoka kwenye kadi za karatasi na kwenda kwenye kadi za kielektroniki Ili kutengeneza kanzi data itakayowasaidia katika kazi zao.
Hayo yamesemwa Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa CCWT Taifa Mrida Mshote Marocho wakati Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mkutano wa uzinduzi wa kadi hizo Oktoba 28 chinangali park Jijini humo.
"Kwasababu sasa tunahitaji kujua wafugaji wetu wanapatikana maeneo gani,na idadi yao niwangapi Kwa sababu kumekuwepo na changamoto nyingi ya migogoro kati ya wakulima na wafugaji na watumiaji wengine wa Ardhi wakiwemo wahifadhi,
Sisi kama chama tumekaa tukaangalia kwamba tukipata kanzi data hiyo itatusaidia kwa kiwango kikubwa sana na tunatamani siku ya uzinduzi wafugaji wengi waweze kujitokeza,"alisema
Aidha alisema kuwa mkutano huo utakwenda kuongeza uwajibikaji na uwazi katika kusimamia rasilimali za chama hicho.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mipango na fedha Taifa(CCWT)Mathew Masele alisema kuwa baada ya uzinduzi huo wameaguza Kila Kanda watakuwa na vijana 2 Kila Kata kwaajili ya kufanyiwa mafunzo na kukabidhiwa vishikwambi kwaajili yakwenda kuwaorodhesha wanachama katika maeneo yao.
"Vijana hao wawili Kwa Kila Kata Nchi nzima Kila ijumaa watakuwa wanatumia taarifa na kituo kikuu cha kupokea taarifa hizo ni hapa dodoma,pia vitambulisho vitatoka hapa Kila ijumaa ya wiki vitambulisho vitakuwa vinarudi kwenye Kanda na tayari kwa kugaiwa Kwa wanachama kwaiyo tumejipanga Kwa hilo,"alisema.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya malisho na migogoro ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi Tanzania Sir George Kifuko alisema kuwa wafugaji wanasahiliwa ili watambulike na itasaidia wao kujieleza Serikali idadi ya wafugaji waliopo pamoja na maeneo yao na changamoto zinazowakabili.
"Kama chama Cha wafugaji tumejipanga kuhakikisha tunatatua migogoro yao wafugaji na tunachotaka sasa baadhi ya viongozi wachache ambao wanavunja kiapo Chao badala kusuruhisha migogoro wao wanakuwa sehemu ya tatizo,
Tulitegemea kwamba watoto wakigombana wanapokwenda Kwa baba wakasuruhushwe na sio kuwa upande mmoja Kwa mtu aliyepigwa,sisi tunatamani viongozi wetu wa Serikali kuangalia changamoto na kuwa sehemu ya kutatua migogoro sio nayeye kuwa sehemu ya mgogoro,"alisema.
Huku mwanasheria wa CCWT Adv.Mathwe Mtemi alisema kuwa lengo kubwa la chama icho ni pamoja na kutetea maslahi na haki za wanachama ambao ni wafugaji kupitia lengo hilo chama kinaidara ya wakili ili kutetea haki za wanachama wote.
"Moja Kati ya majukumu makubwa tunatoyafanya ni pamoja na kuangalia hasa zile sheria korofi au zinazokandamiza haki za wafugaji Tanzania ni wazi kwamba kuna baadhi ya Wilaya kunachangamoto za wafugaji na wakulima Kwa mfano tunduru,kilosa,bagamoyo,mvomero na Wilaya zingine nyingi,
Sisi kama Chama hasa wanasheria tumejipanga kuja na andiko litakalokwenda Kwa mwanasheria Mkuu wa Serikali na kumueleza kuhusu sheria ambazo zinamkandamiza mfugaji,"alisema.
No comments:
Post a Comment