Wednesday, April 19, 2023

WAZIRI BASHUNGWA AFANYA MAZUNGUMZO WA WANAVYUO KUTOKA KARAGWE NA KYERWA.

 








Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Mhe. Innocent Bashungwa amekutana na kufanya mazungumzo na Wanafunzi wa Vyuo vikuu wanaotokea Wilaya za Karagwe na Kyerwa waliopo Mkoani Dodoma walio katika umoja wao unaofahamika kama KARSA DODOMA.

Wanafunzi hao wa Vyuo wakiongozwa na Mwenyekiti wa KARSA, Ndugu Salius Sospeter wamepafa fursa hiyo wakati walipotembelea Bunge la Tanzania kwa ajili kupata mafunzo ya elimu juu ya Shughuli zinazoendea Bungeni Jijini Dodoma, leo Aprili 19, 2023.

Katika Mazungumzo hayo yaliyofanyika Katika Ukumbi wa Bunge wa Msekwa, Wanafunzi hao wamepata fursa ya kujifunza pia kuwasilisha hoja na maoni yao mbalimbali ambayo Waziri Bashungwa alipata fursa ya kutolea ufafanuzi.

Pamoja na Mambo mengine, Waziri Bashungwa ametumia nafasi hiyo kueleza kazi kubwa inayiendelea kufanywa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuwahasa kutumia fursa mbalimbali ambazo zinaendelea kutolewa na Serikali ya awamu ya sita.

No comments:

Post a Comment